I am Bad Man

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“I am Bad Man”
“I am Bad Man” cover
Single ya Dknob akiwa na Cannibal
Imetolewa 1 Desemba 2008
Muundo CD single
Imerekodiwa 2008
Aina Hip hop
Urefu 3:40
Studio Vinnice Records
Mtunzi Dknob
Mtayarishaji Villy
Mwenendo wa single za Dknob akiwa na Cannibal
Dear Mtoto
(2008)
I am Bad Man

I am Bad Man ni single pekee ya mwimbaji-rapa wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania - Dknob. Single ilitolewa ikiwa kama wimbo wa ziada kutoka kwenye albamu ya Bomoa Mipango, lakini haikuweza kuwa kwa kufuatia kuchelewa kwake katika kutoka. Single ilitolewa mnamo tar. 1 Desemba ya mwaka wa 2008, ikiwa imemshirikisha msanii machachari wa hip hop kutoka Kenya Bw. Cannibal.

Maelezo ya wimbo[hariri | hariri chanzo]

Kiitikio chacke kinasema

I'm Bad Man, hapo ulipo simama sipo, stay away from me
I'm bad man, chips hailiwi kwa kijiko
stay away from me, I'm bad man.

Single inaelezea namna Dknob anayvowabamba wapenzi zake, huku akiwa ana wahusia wale wanaojifanya hawataki kumkubali na kusema ya kwamba: Stay Away From Me kwa sababu wenzako wananiogopa kama UKIMWI.

Video yake[hariri | hariri chanzo]

Video yake ilianza kutengenezwa mwishoni mwa mwezi Septemba katika mwaka wa 2008, ikiwa chini ya uongozi wake mtayarishaji, mwongozaji, na mwandikaji muswaada andishi wa Visual Lab Bw. Adam Juma. Kwa pamoja walifanikisha kuifanya video hiyo na kuja kuitoa rasmi kunako tar. 24 Novemba ya 2008, halafu baada ya wiki moja ikatoka audio ya single yake. Waliouza sura kwenye video hii ni mwanadada Melisa ambaye pia msanii kutoka Kenya, G. Gangsta kutoka katika kundi la zamani la hip hop la F.D.C, na baadhi ya wasanii wa Mj Records nao walionekana kwenye video hiyo.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]