Nenda kwa yaliyomo

Miikka Mwamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miikka Mwamba
Miikka Mwamba.
Miikka Mwamba.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Miikka Aleksanteri Kari
Amezaliwa 16 Oktoba 1971 (1971-10-16) (umri 53)
Asili yake Finland
Aina ya muziki Hip hip
R&B
Dansi
Pop
Kazi yake Mtayarishaji
Studio Mwamba Productions
FM Studio
Kokwa Records
Tovuti Mwambaproductions.com

Miikka Aleksanteri Kari (anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Miikka Mwamba; amezaliwa Helsinki, Ufini, 16 Oktoba 1971) ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Ufini-Tanzania. Miikka Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri sana kwa nchi ya Tanzania, na ameweza kujibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.

Jina lake ni Miikka Kari, ila Kari alibadili iwe kwa Kiswahili na tafsiri yake ni Mwamba, hivyo aliamua kujiita Miikka Mwamba[1]

Miikka aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice, Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi wa kutoka Tanzania.

Miikka alihitimu elimu yake ya msingi na sekondari Lohja, ambacho ni chuo cha sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) alisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA) alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.

Nyimbo zilizotamba

[hariri | hariri chanzo]
  • Julieta - Dully Sykes (2000)
  • Athumani Mlevi - Solid Ground Family (2001)
  • Baby Gal - Mad Ice (2002)
  • Tupa Mawe - Zahrani na Complex (2001)
  • Twenzetu - Chegge, Ferouz na Mh Temba (2005)
  • Elimu Mitaani.com - Dknob (2003)
  • Kitu Gani - Dknob (2007)
  • Tamara + ni wewe - Hard Mad
  • Eno maiki - Ziggy Dee (Uganda)
  • Nakupenda Mpenzi - Dudu Baya
  • get down - Prezo ft Naziz (Kenya)
  • Twenzetu - Chege
  • Baby Gal + wange - Mad Ice
  • Maria Salome - Saida Karoli
  • Kamanda + barua - Daz Nundaz
  • wanoknok + Taswira + dingi - Mandojo na domokaya
  • Picco - Kikongwe
  • Kwenye Chati - Balozi
  • Mtoto wa geti kali - Inspector Haroun
  • Elimu mtaani + sauti ya gharama - D knob
  • Mkiwa - K sal ft Ferooz
  • Salome + Julieta + Hi - Dully Sykes
  • Raha tu - AY
  • Mambo vipi - Mchizi Mox
  • Solid Ground Family - Bush party
  • Nini mnataka mazee- Pig black

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. Mika Mwamba ndiye Producer mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza beats kali kuwahi kutokea kwenye historia ya Bongofleva | JamiiForums