Nenda kwa yaliyomo

Amani Temba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mh Temba)
Amani James Pausen Temba
Mwanamuziki Temba
Mwanamuziki Temba
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Mheshimiwa Temba
Nchi Tanzania
Alizaliwa 1980
Aina ya muziki Hip Hop na Bongo Flava
Kazi yake Mwanamuziki, Mchezaji Mpira wa Kikapu
Miaka ya kazi mn. 1999 -
Ameshirikiana na Dully Sykes, Ray C nk.
Ala Muimbaji
Kampuni Bongo Records, Mandugu Digital

Amani James Pausen Temba au "Mheshimiwa Temba" maarufu kama Mheshimiwa Temba ni Mwanamuziki wa Rap na Hip Hop Kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania, Na pia ni Mwanachama Kiongozi wa Tmk Wanaume Familia yenye makazi yao huko Temeke jijini Dar es Salaam Tanzania, Mheshimiwa Temba alizaliwa mwaka 1980 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Temeke na baadaye kujiunga na shule ya sekondari ya Nuru Yakini ambako alisoma kwa miaka miwili kabla ya kuhamia sekondari ya Makongo. Alisoma Makongo kwa muda wa wiki moja tu na kwenda kujiunga na sekondari nyingine inayomilikiwa na Jeshi ya Jigetemee baada ya kupata ofa ya kusomeshwa bure na uongozi wa shule hiyo enzi hizo ukiwa chini ya Luteni kanali Fabian Massawe ambaye sasa ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Maisha ya Muziki

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni alitokea kwenye kundi flani liitwalo "Manduli Mobb" walifanya nyimbo kadha wa kadha ikiwemo ile ya 'Maskini Jeuri' walishirikiana na 'Juma Nature' hiyo ilikuwa mwaka 2000. Badae kundi lika tawanyika na kila mtu kuanza kufanya kazi za muziki akiwa peke yake na sio na kundi tena. Alioanza kutoa nyimbo yake peke alikuwa "Bwana Mkubwa" baadae Mheshimiwa Temba nae akatoa nyimbo yake ya kwanza ilioitwa "Nakumaindi" ikiwa ni mwaka 2001 mwishoni ambayo ilitayarishwa na muuandaaji Papa maarufu kama Bonny Lavu.

Miaka iliyo fuatia akajiunga na Tmk Wanaume enzi hizo Juma Nature ajatoka kwenye kundi la Tmk Wanaume. Mheshimiwa Temba akatoa nyimbo nyingine iliyoitwa "Nampenda Yeye" ambayo aliimba na Dully Sykes nayo ilivuma sana na kumpa heshima kubwa katika medani ya Muziki wa Tanzania baadae akawa anapata ushirika mwingi tu na wasanii mbali mbali.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amani Temba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.