Nenda kwa yaliyomo

Tmk Wanaume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii ni Kasha ya Albamu ya Tmk Wanaume Enzi Hizo Hawaja Sambaratika

TMK Wanaume Family ni kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam Tanzania. Kundi lilianzishwa rasmi mnamo Septemba 16 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo Ugali na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni Kutokea Kiumeni na Ndio Zetu. Wasanii wa kundi baadhi kabla ya wengine kujiengua ni Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chegge, Yp, Y Dash, na wengineo, halafu baada ya kutengana kukawa na "Tmk Wanaume Halisi" na Tmk Wanaume. Tmk Wanaume kiongozi wa kundi ni Mh Temba na Chegge wakati Tmk Wanaume Halisi kiongozi wa kundi ni Juma Nature na Inspector Haroun.[1]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tmk Wanaume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.