Comair

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Comair

Comair ni ndege iliyo na makao yake nchini Afrika Kusini. Makao ya ndege zake ni kwenye Uwanja wa ndege wa OR Tambo mjini Johannesburg pamoja na makao mengine kwenye nyanja za ndege za Cape Town na Durban.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ndege hii ilianza kufanya kazi mnamo 14 Julai 1946 kwa jina la Commercial Air Services. Ilianzishwa na AC Joubert, JMS Martin, L Zimmerman na JD Human. Safari za ndege kati ya Rand Airport, Johannesburg na Durban zilianza 1948, kwa kutumia ndege aina ya Cessna. Pamoja na safari hizi nchini Afrika Kusini, ilianzisha safari za nje ya nchi hadi miji kama Gaborone na Harare.[1] Kampuni hii iliwekwa kwenye soko la hisa la Johannesburg mnamo 1998. Ndege hii inamilikiwa na meneja (25%), makampuni na umma (52%), British Airways (18%) na wafanyikazi (5%). Hadi Machi 2007, ilikuwa na wafanyikazi 1,447.

Mnamo 2007, Comair ilianzisha kulula.com ambayo ni ndege inayosafirisha watu kwa bei rahisi.

Miji inayosafiria[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya safari za Comair

Ndege zake[hariri | hariri chanzo]

Hadi 25 Septemba 2009, Comair ilikuwa na ndege: [2]


Mdege Juma Oda
Boeing 737-200 3 0
Boeing 737-300 12 0
Boeing 737-400 7 0
Comair mnamo 1970[3]
Ndege Jumla Oda Maelezo
Cessna 401 1 0
Douglas DC-3 4 0
Jumla 5 0

Ajali[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Nachi 1, 1998 ndege ya Comair Flight 206 ilipata ajali mjini Johannesburg na wasafiriwa wote 17 walikufa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-04-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.
  2. [1]
  3. [2]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]