Livingstone (mji)
Livingstone ni mji na makao makuu ya mkoa wa Kusini wa Zambia, kando ya mto Zambezi, wenye wakazi 110,000 (2005).
Mji ni kitovu cha utalii wa Maporomoko ya maji ya Victoria Falls upande wa Zambia. Pia ni kituo cha mpakani kwenye daraja la Zambezi kwenda Zimbabwe.
Mji ulianzishwa penye mpito wa mto Zambezi, kidogo juu ya maporomoko, mwaka 1897. Jina lake limetolewa kwa heshima ya mmisionari na mpelelezi David Livingstone.
Ulikuwa makao makuu ya kampuni ya Cecil Rhodes iliyotawala Rhodesia ya Kaskazini, baadaye mji mkuu wa koloni hadi mwaka 1935 serikali ilipohamishwa kwenda Lusaka.
Baada ya uhuru wa Zimbabwe, watalii wengi waliotaka kuona maporomoko walipendelea kukaa upande wa Zimbabwe lakini tangu miaka ya nyuma matatizo ya kiuchumi na ya kisiasa ya Zimbabwe yalisababisha kupanda kwa idadi ya watalii upande wa Zambia.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Zambia National Tourist Bureau page
- Livingstone Tourism website Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Zambia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Livingstone (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |