Nenda kwa yaliyomo

Gaborone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Gaborone

Gaborone ni mji mkuu wa Botswana ikiwa na wakazi 186,000 (mwaka 2001). Iko kusini-mashariki ya nchi.

Mji huu ulianzishwa kwenye makao ya chifu Kgosi Gaborone wa BaTlokwa. Waingereza walijenga kituo kidogo cha kiutawala kando ya kijiji cha chifu. Makao haya madogo yalikua ghafla wakati wa uhuru wa Botswana ilipoamuliwa kujenga mji mkuu mpya. Botswana iliwahi kuwa na mji wake mkuu wa kikoloni ndani ya eneo la Afrika Kusini katika mji wa Mafeking ilitawaliwa na Uingereza kwa jina la "Bechuanaland Protectorate."

Uhuru ulipokaribia viongozi waliona haja ya kuwa na mji mkuu ndani ya Botswana wakaamua kupanua Gaborone.

Katika muda mfupi wa miaka mitatu mnamo 1965 - 1967 pekee mji mpya ukajengwa mwenye majengo ya bunge, serikali, kituo cha umeme, shule, hospitali, polisi, posta, benki, maduka, kanisa, hoteli, kiwanda cha bia, uwanja wa michezo na nyumba 1000.

Leo hii Gaborone ni mji wa kisasa kabisa inayoonyesha maendeleo ya kiuchumi wa Botswana. Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini (Southern African Development Community (SADC)) ina makao makuu yake Gaborone. Kuna pia Chuo Kikuu cha Botswana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Bruce Bennett, "A note on place names, historical terms, etc.", [1]