Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli
Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (kwa Kiingereza: Tanzania Military Academy; kifupi: TMA) ni chuo cha maafisa wa kijeshi kilichopo katika wilaya ya Monduli, mkoa wa Arusha nchini Tanzania.[1] TMA ni moja kati ya taasisi muhimu inayotoa mafunzo ya jeshi[2]. Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya kijeshi kwa maofisa toka nchi mbalimbali zinazoizunguka Tanzania.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilijengwa kwa msaada wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kufunguliwa rasmi na rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1976. Kwa mara ya kwanza chuo cha TMA kilikuwa kikijulikana kama Chuo cha Taifa cha Uongozi kabla ya kubadilishwa jina lake mwaka 1992 baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi.[3] Kwa miaka mingi, chuo cha TMA kimekuwa kikitoa mafunzo kwa maafisa toka nchi za Kenya, Lesotho, Shelisheli, Afrika Kusini, Zambia na Uganda.[4]
Wanafunzi maarufu
[hariri | hariri chanzo]- Jakaya Kikwete, 1976[5]
- Katumba Wamala
- Elly Tumwine
- Joseph Semwanga
- Makongoro Nyerere
- Yusuf Makamba
- Venance Salvatory Mabeyo
- John Mutwa
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Nkwame, Marc. "Kikwete awards outstanding female army pilot", 15 July 2013. Retrieved on 19 November 2013. Archived from the original on 2013-10-05.
- ↑ "EA Defence Forces To Hold First-Ever Joint Field Training Exercise in Arusha and Tanga". East African Community. 1 Septemba 2009. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kikwete Commissions 425 Cadres AT Monduli", 24 January 2011. Retrieved on 20 November 2013. Archived from the original on 2013-11-20.
- ↑ "Seychelles cadets reap rewards of Monduli military course", August 26 – September 1, 2006. Retrieved on 20 November 2013. Archived from the original on 2015-09-23.
- ↑ "President Kikwete lays foundation for Military Academy library", Dec 3–7, 2011. Retrieved on 19 November 2013. Archived from the original on 2015-09-23.