Chris Rock

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chris_Rock_WE_2012_Shankbone

Chris Rock ni mchekeshaji maarufu katika nchi ya Marekani. Anajulikana kama “stand-up comedian” kwa vichekesho yake kuhusu ubaguzi wa rangi. Chris Rock ni mwigizaji, mwandishi, mtayarishaji na mwongozaji wa filamu pia.

Maisha ya zamani[hariri | hariri chanzo]

Christopher Julius Rock ni jina lake kamili walimtoa na wazazi wake Rosalie na Julius Rock. Mama yake alikuwa mwalimu wa watu wenye udhaifu wa akili. Baba yake alikuwa dereva wa gari na mtu wa kutoa magazeti. Chris Rock (jina lake la kisanii) alizaliwa Februari 7, 1966, katika nchi ya Amerika, jimbo la South Carolina na mji wa Georgetown. Baada ya kuzaliwa, wazazi wake walihamia jimbo la New York mji wa Brooklyn. Chris Rock ni mtoto ya kwanza. Wazazi wake walikuwa na watoto saba, wavulana sita na msichana mmoja. Wadogo zake watatu Tony, Kenny na Jordan pia wako kwenye biashara ya burudani. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba Chris Rock aliacha shule. Baada ya kuacha shule alianza kufanya kazi katika vilabu vidogo vya uchekeshaji. Alipofanya kazi katika vilabu, Rock aligunduliwa na Mchekeshaji mwingine maarufu, Eddie Murphy. Rock aliigiza katika filamu za Eddie Murphy kama vile "Beverly Hills Cop II" na "I'm Gonna Git You Sucka".

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya Chris Rock ilianza kufanya vizuri alipoajiriwa kuwa kwenye Saturday Night Live(SNL). Alifanya kazi kwenye SNL kwa miaka mitatu kutoka 1990 hadi 1993. Aliondoka baada ya miaka mitatu na kuanza kufanya kazi kwenye tamthilia "In Living Color". Tamthilia kiliacha mwezi mmoja baada ya Chris Rock kujiunga. Chris Rock baadaye alitengeneza tamthilia yake ya kwanza ya uchekeshaji iliyoitwa "Big Ass Jokes". Alitengeneza tamthilia mnamo 1994 na ilishinda Tuzo la CableACE. Alitengeneza tamthilia yake ya mbili ya uchekeshaji ilichoitwa “Bring the Pain”. Aliumba tamthilia huo mnamo 1996 na ilishinda tuzo mbili za Emmy. Mnamo 1999 na 2004 Chris Rock aliumba tamthilia mengine mawili ya uchekeshaji iliyoitwa " Bigger & Blacker " na " Never Scared ". Baada ya hapo alizingatiwa "mtu mcheshi zaidi Amerika". Aliumba tamthilia yake ya kwanza ya mazungumzo inayoitwa "The Chris Rock Show". Kazi yake ya televisheni ilimshindwa jumla ya Tuzo tatu za Emmy na uteuzi 15. Kazi yake yenye mafanikio zaidi iliitwa "Everybody Hates Chris". Tamthilia inatokana na maisha ya Chris Rock wakati alipokuwa mtoto. Tamthilia yake iliteuliwa kwa Tuza la Golden Globe mnamo 2006 kwa mfululizo Bora wa TV. Alishinda mnamo 2006 "Tuzo la Peoples Choice" kwa vichekesho vinavyopenda vya Televisheni na tuzo mbili za Emmy.

Maelezo kuhusu Chris Rock[hariri | hariri chanzo]

  • Chris Rock aliwahi kushikilia rekodi ya dunia kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi wakati wa tamthilia la vichekesho alipotumbuiza mbele ya watu 15,900 huko London mnamo mwezi wa tano mwaka la 2008.
  • Chris Rock hakujifunza kuogelea hadi alipokuwa na umri wa miaka hamsini na tano Sasa anaishi katika jimbo la New Jersey mji wa Alpine

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]