Bukoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bukoli ni kata ya Wilaya ya Geita katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 16,345 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 30121.[2]

Hali wa maisha[hariri | hariri chanzo]

Bukoli ni mji mzuri kwa hali ya hewa iliotulia, wakazi wake wana ushirikiano mkubwa katika masuala ya kijamii.

Gharama za maisha katika mji wa Bukoli ziko chini ukilinganisha na mahali kama Nyarugusu, Geita Mjini, kwani wakazi wengi wa Bukoli ni wakulima. Wanalitumia vizuri daraja lisilokauka mwaka mzima kulima bustani na mazao yakomaayo mapema kwa wingi hivo upatikanaji wa chakula kwa wingi na bei nafuu.

Katika mji wa Bukoli kuna shughuli mbalimbali za uchumi kama jineri ya kusafisha mbegu za pamba kwa ajili ya kutoa mafuta. Jineri hizi huufanya mji wa Bukoli kuchangamka na wakazi wake kupata ajira kwa urahisi.

Mafanikio ya Bukoli Sekondari[hariri | hariri chanzo]

Katika mji huo kuna sekondari moja, iitwayo Bukoli Secondary School. Shule hii imefanya vizuri katika mitihani ya taifa kwa miaka sasa. Imekuwa kama shule baba kwa shule kama Nyarugusu Sekondari, Kamena Sekondari, Ntono Sekondari, Nyaruyeye sekondari, Butobela sekondari.

Bukoli sekondari ilianza rasmi mwaka 1993 kama shule ya wazazi, baadae ilichukuliwa na serikali. Toka ilipochukuliwa na serikali wanafunzi wakaanza kwenda form five katika shule mbalimbali, hii ni kutokana na serikali kuleta waalimu waliodhamilia kufundisha kwa nguvu na kujitoa kwa moyo wote, mnamo mwaka 2002 Msela Mbumbuli ndiye alikuwa mwanafunzi wa kwanza kupata division one point 17. Mwaka uliofuata 2003 Lesa Simoni pamoja na mhamiaji (mwaka wa form 4) Maziku Faustine ndio waliopata division one za 12 kwa Maziku Faustine, na 17 kwa Lesa Simon. Pia kiranja mkuu Mussa Kasanga, Tumaini Shibitali na wengine wawili walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano. Mwaka 2005 kulikuwa na division one watatu. Joseph Fred alipata division 1 ya point 10; Abdallah Mwita division 1 ya point 14, na Bahati Albert division one ya point 15 ambazo mpaka leo hakuna mwaka uliovunja record hiyo. Hii ni changamoto kwa vijana wanaosoma shule ya Bukoli secondary kuongeza bidii ili kufanya vizuri zaidi. kwani waliofaulu kwenda kidato cha tano na sita wote walifika vyuo vikuu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Geita Region – Geita District Council
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
Kata za Wilaya ya Geita Vijijini - Mkoa wa Geita - Tanzania

Bugalama | Bugulula | Bujula | Bukoli | Bukondo | Busanda | Butobela | Butundwe | Chigunga | Isulwabutundwe | Izumacheli | Kagu | Kakubilo | Kamena | Kamhanga Kaseme | Katoma | Katoro | Lubanga | Ludete | Lwenzera | Magenge | Nkome | Nyachiluluma | Nyakagomba | Nyakamwaga | Nyalwanzaja | Nyamalimbe | Nyamboge | Nyamigota | Nyamwilolelwa | Nyarugusu | Nyaruyeye | Nyawilimilwa | Nzera | Rwamgasa | Senga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.