Bobi Wine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bobi Wine mwaka 2019.

Robert Kyagulanyi Ssentamu (anajulikana kwa jina la kisanii kama Bobi Wine; alizaliwa 12 Februari 1982) ni mwanasiasa, mwimbaji, mwigizaji na mfanyabiashara wa Uganda.[1] ni kiongozi katika harakati maarufu dhidi ya Rais Yoweri Museveni na harakati hizo hujulikana kama People Power, Our Power.[2] mwaka 2019, alitangazwa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Uganda.

Kyagulanyi alizaliwa katika hospitali ya Nkozi, ambapo mama yake aliwahi kufanya kazi.[3] alikulia katika mji mkuu wa Uganda Kampala .[4]

Kyagulanyi alisoma katika shule ya Kitante Hill School, ambapo alipata cheti cha elimu yake ya msingi mwaka 1996. Mwaka 1998 alihitimu elimu ya upili katika shule ya Kololo Senior Secondary School na kupata cheti, kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere alikosomea muziki na sanaa ambapo alihitimu kwa ngazi ya diploma mwaka 2003, mnamo mwaka 2016 Kyagulanyi alirudi tena chuo kikuu na kujifunza sheria katika International University of East Africa (IUEA).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Editor. "Bobi Wine Biography, Early Life, Age, Family, Education, Career And Net Worth". Information Guide Africa. Iliwekwa mnamo 2021-01-15. 
  2. URN. "Can 'People Power' change Uganda's political fortune?", The Observer - Uganda. (en-gb) 
  3. Mazinga, Mathias (14 June 2016). "Cardinal Wamala, singer Bobi Wine set for Nkozi Hospital marathon". New Vision. Kampala. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-13. Iliwekwa mnamo 12 November 2018.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. Ariba, Caroline (6 September 2012). "Bobi giving back to the hands that lifted him up". New Vision. Kampala. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-10. Iliwekwa mnamo 11 July 2017.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bobi Wine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.