Bahaʼullah
Bahá'u'lláh, (12 Novemba 1817 - 29 Mei 1892) ni mwanzilishi wa Dini ya Kibaha'i na kulingana na wabaha'i ni Mdhihirishaji wa Mungu wa enzi hii. Alizaliwa Iran. Alizaliwa katika familia ya kiungwana huko Persia na alihamishwa kwa sababu ya kufuata dini ya Bab. Mnamo 1863, huko Iraq, alitangaza kwa mara ya kwanza dai lake la kuwa Mdhihirishaji wa Mungu na alitumia maisha yake yaliyobaki katika Dola la Ottoman akiwa kifungoni. Mafundisho yake yanahusu kanuni za umoja na ufanyaji upya wa dini, ambayo yanajumuisha maendeleo ya maadili na kiroho hadi utawala wa ulimwengu.[1]

Bahá'u'lláh alilelewa bila elimu rasmi lakini alikuwa amejaa hekima ya kiasili na alikuwa mtu wa kidini. Familia ya Bahá'u'lláh ilitokea jimbo la Māzandarān wilaya ya Nur, ambayo huunda pwani ya kusini ya Bahari ya Caspian. Ilikuwa ni desturi kwa watu mashuhuri wa Nur kufanya kazi kwa serikali huko Tehran kama wakusanya ushuru, walipaji wa jeshi, na maafisa wengine wanaoaminika. Baba yake Bahá'u'lláh, Mirza Abbas Nuri, alikuwa afisa wa cheo cha juu mahakamani.[2] Familia yao ilikuwa na utajiri mkubwa, na alipofikisha miaka 22, Bahá'u'lláh alikataa nafasi serikalini, badala yake akasimamia mali za familia na akatoa muda na pesa kwa ajili ya misaada.[3] Katika umri wa miaka 27 alikubali ujumbe wa Báb na kuwa mmoja wa wafuasi wenye sauti kubwa wa harakati ya dini mpya iliyoeneza kufanya upya kwa sheria za Kiislamu, jambo lililokumbana na upinzani mkali. Katika umri wa miaka 33, wakati wa jaribio la serikali la kuharibu harakati hiyo, Bahá'u'lláh alinusurika kifo, mali zake zilikamatwa, na alifukuzwa kutoka Iran. Kabla tu ya kuondoka, akiwa amefungwa katika gereza la Siyah-Chal, Bahá'u'lláh alidai alipokea ufunuo kutoka kwa Mungu, akioneshwa mwanzo wa utume wake wa kimungu.[4] Baada ya kuhamia Iraq, maafisa wa Irani, kwa mara nyingine tena, walijawa na hasira dhidi ya Bahá'u'lláh. Jambo hili lilipelekea kwa maafisa hawa kutuma ombi kwa serikali ya Uturuki kumpeleka mbali. Alikaa Constantinople kwa miezi kadhaa, ambapo maafisa walipinga madai yake ya kidini na kumuweka chini ya kifungo cha nyumbani kwa miaka minne huko Edirne, ikifuatiwa na kifungo cha miaka miwili cha mateso katika mji wa gereza 'Akka'. Vizuizi vyake vilipungua hatua kwa hatua hadi miaka yake ya mwisho ambapo alienda kuishi katika eneo karibu na 'Akka' kwa uhuru. Katika maisha yake yote Bahá'u'lláh alipatwa na majaribu mengi, alipitishwa mateso, mipango ilifanywa na viongozi wa kidini dhidi yake.[2]
| Baháʼu'lláh | |
|---|---|
| Amezikwa | 32°56′36″N 35°05′32″E / 32.94333°N 35.09222°E |
| Watoto |
|
Bahá'u'lláh alieleza wazi katika barua zake kwamba mwakilishi wa Mungu hupitia mateso kama hayo:
Uzuri wa Kale amekubali kufungwa kwa minyororo ili jamii ya wanadamu iweze kuachiliwa kutoka kwenye utumwa wake, na amekubali kufanywa mfungwa ndani ya Ngome hii kuu kabisa ili ulimwengu mzima uweze kufikia kwenye uhuru wa kweli. Amekunywa mashinda ya kikombe cha huzuni, ili watu wote wa dunia waweze kufikia kwenye shangwe ya kudumu, na kujazwa na furaha. Hii ni kwa huruma ya Bwana wenu, Mwenye huruma, Mwenye rehema Kabisa. Tumekubali kutwezwa, Enyi waumini katika Umoja wa Mungu, ili muweze kutukuzwa, na tumepata mateso mengi, ili muweze kusitawi na kushamiri. Yeye Ambaye amekuja kuujenga upya ulimwengu mzima, tazama, jinsi wale ambao wamefanya washiriki wa Mungu walivyomlazimisha kukaa ndani ya miji yenye ukiwa kabisa.[5]
Bahá'u'lláh alifunua angalau nyaraka 1,500, ambazo zingine ni ndefu kama vitabu na ambazo zimepewa tafsiri angalau katika lugha 802. Baadhi ya mifano mashuhuri ni pamoja na Maneno Yaliyofichwa, Kitabu cha Yakini, na Kitab-i-Aqdas (Kitabu Kitakatifu Kabisa). Baadhi ya mafundisho yake yanahusiana na asili ya Mungu na maendeleo ya roho, wakati mengine yanazungumzia mahitaji ya jamii, wajibu wa kidini wa wafuasi wake, au muundo wa taasisi za kibahá'í ambazo zitashughulikia kufundisha dini.[6] Aliona wanadamu kimsingi kama viumbe wa kiroho na aliwasihi watu binafsi kukuza sifa za kiroho na kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiroho.[7]
Maisha ya Awali

Bahá'u'lláh, jina lenye maana ya "Utukufu wa Mungu" katika Kiarabu, alizaliwa tarehe 12 Novemba 1817 huko Tehran, Iran. Jina alilopewa alipozaliwa lilikuwa Hussein Ali, na alikuwa ni mwana wa waziri tajiri wa serikali, Mirza Abbas Buzurg-i-Nuri. Baba yake, Mirza Abbas-i-Nuri, ambaye alijulikana kwa jina la Mirza Buzurg[8], aliwahi kuwa waziri wa mtoto wa kumi na mbili wa Fath-Ali Shah Qajar, Imam-Verdi Mirza. Mama yake aliitwa Khadijeh Khanum.[9] Familia hii ilionyesha uhusiano wao na koo kuu za kifalme za zamani za Iran. Bahá'u'lláh aliishi maisha ya kifahari kama kijana, na alipata elimu iliyojikita zaidi katika uandishi wa maandiko, upandaji farasi, ushairi wa kilasiki, na upiganaji wa upanga. Wanahistoria wameunganisha ukoo wake na Ibrahim, kupitia wake zake wote wawili, Keturah[10] na Sara, Nabii Zoroaster, Yese baba wa Mfalme Daudi, na Yazdegerd III, ambaye alikuwa mfalme wa mwisho wa Milki ya Sasanian[8].
Bahá'u'lláh alimuoa Asiyeh Khanum, binti wa familia ya kiungwana huko Tehran, mwaka 1835, yeye akiwa na umri wa miaka 18 na mkewe akiwa na umri wa miaka 15[11]. Katika miaka yake ya mwanzo baada ya kufikisha umri wa miaka ishirini, Bahá'u'lláh alikataa maisha ya upendeleo waliyokuwa nayo watu wa ukoo wake na kugawa rasilimali zake pamoja na muda wake kwa kazi nyingi za misaada. Kwa sababu hii, alipata umaarufu kama "baba wa maskini".[3]
Dini na Utambuzi wa Bab

Mwezi Mei 1844, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 24 kutoka Shiraz, Sayyid Mirza Ali-Muammad, alitikisa Iran nzima kwa kutangaza sio tu kwamba yeye ndiye aliyeahidiwa katika dini ya Uislamu (Qa'im au Mahdi) bali pia kuwa mjumbe mpya kutoka kwa Mungu.[12] Alijichukulia cheo cha "Bab" (kwa Kiarabu: "mlango"), ili kuonesha nafasi yake kama "mlango wa elimu ya kiungu", na kama mwalimu mkubwa aliyetumwa na Mungu, ambaye alikuja kutayarisha njia yake.[13] Mara tu baada ya kutangaza ujumbe wake ya kiroho kwa Mulla Husayn, Bab alimuagiza ujumbe kwenda kwa mtu maalum huko Tehran ambaye Mungu angemwongoza kumpata. Baada ya kujua juu ya Baha'u'llah kupitia rafiki, Mulla Husayn alihisi akivutwa kumpelekea Baha'u'llah ujumbe aliokuwa amekabidhiwa - alipomwandikia Bab kuhusu jambo hili, Bab alifurahia sana na habari hiyo.[14] Baha'u'llah alipopokea ujumbe huo alikuwa na umri wa miaka 27, alikubali ukweli wa ujumbe wa Bab mara moja na kusimama kuushiriki na wengine.[11] Umaarufu wa Baha'u'llah kama mtu mashuhuri katika mkoa wake wa asili, Nur, ulimpa nafasi nyingi za kufundisha dini ya Babi, na safari zake zikavutia watu wengi, wakiwemo makasisi wa Kiislamu, kwenye dini hiyo mpya.[15] Nyumba yake huko Tehran iligeuka kitovu cha shughuli na alitoa msaada wa fedha kwa ukarimu kwa ajili ya shughuli za dini hiyo.[16] Katika majira ya joto ya 1848, Baha'u'llah alihudhuria na kuandaa mkutano katika Badashat, mkoa wa Khorasan, ambapo wafuasi 84 wa Babi walikutana kwa siku 22. Huko Badashat, alichukua jina la Baha[17], ambalo maana yake ni "utukufu" na "Baha'u'llah" lina maana "Utukufu wa Mungu". Pia alitoa majina ya kiroho mapya kwa watu wengine wote waliokuwepo; baada ya hapo Bab aliwasiliana nao kwa majina hayo. Baada ya mkutano huo, mwanafunzi wa kike maarufu zaidi wa Bab, Tahirih, alipokamatwa, Baha'u'llah alijaribu kumtetea. Baadaye alifungwa kwa muda na kuadhibiwa kwa kupigwa mwili wake.[18]
Dini ya ubabi ilienea haraka katika Uajemi na idadi ya wafuasi wake iliongezeka kwa kasi. Hii ilisababisha upinzani mkubwa kutoka kwa viongozi wa kidini wa Kiislamu, ambao waliogopa kupoteza mamlaka ya kidini na faida zinazohusiana nazo, na kwa upande mwingine, viongozi wa utawala walionesha upinzani kwa sababu waliogopa ushawishi unaoongezeka wa jamii ya Kibabi [19], na kusababisha kampeni za mateso ambazo zilipelekea kuuwawa kwa maelfu ya wababi. Mnamo Julai 1850, Bab aliuawa na kikosi cha askari huko Tabriz akiwa na umri wa miaka 30 [20].
Katika mafundisho yake, Bab alijitambulisha mwenyewe kama wa kwanza kati ya wadhihirishaji wawili pacha wa Mungu waliotumwa na Muumba ili kuanzisha amani ya kudumu, amani ambayo inaashiria kufikia ukomavu wa jamii ya binadamu - wakati ambapo watu wote wataishi kwa umoja kama familia moja ya kibinadamu.[21] Wabaha'i wanaamini kuwa mafundisho ya Bab yaliandaa msingi wa "umoja wa mataifa, maelewano ya dini, usawa wa haki kwa watu wote, na uanzishwaji wa jamii inayoongozwa na sifa za upole, ushauri, uvumilivu, demokrasia, na maadili ya utaratibu wa dunia."[22] Katika mafundisho yote ya Bab kuna maelezo ya "Yule ambaye Mungu atamdhihirisha"[23], mjumbe mkuu aliyetabiriwa ambaye alimuandalia njia. Katika unabii mbalimbali, Bab alisema kwamba mwalimu kutoka kwa Mungu atakayemfuata angeonekana baada ya muda mfupi baada ya kuuwawa kwake kishahidi kulikotarajiwa.[24] Katika moja ya maandiko yake makuu, Bab alisema: "Heri kwa yule ambaye anakazia mtazamo wake kwa Utaratibu wa Baháʼu'lláh, na kumshukuru Bwana wake."[25]
Kufungwa kwao
Kipindi kueleke kuuawa kwa Bab na matukio yaliyofuata, hali ilikuwa ya machafuko kwa Wababi. Viongozi wa Kiislamu waliuchochea umati wa watu dhidi ya vurugu kwa Wababi, Wababi wengi walikataa kuchukua hatua ya mashambulizi dhidi ya wavamizi, bali walichukua hatua za kujilinda[26], lakini kwa kawaida waliuawa. Tarehe 15 Agosti 1852, vijana wawili wa Kibabi walijaribu kumuua mfalme wa Irani ili kulipiza kisasi kwa kuuwawa kwa Bab na wanafunzi wake wakuu. Mara tu Nasiri-din Shah alipopita kwenye barabara mbele ya umati, vijana hao wawili walizuia njia ya mfalme na kujaribu kumuua kwa bunduki ya kupiga ndege. Mfalme alinusurika bila kujeruhiwa vibaya, lakini tukio hili lilisababisha mateso makubwa zaidi dhidi ya Wababi kuliko matukio ya awali.[27] Mfalme aliamuru mauaji ya Wababi, na kila mbabi anayejulikana huko Tehran alikamatwa.[2] Bahá’u’lláh alikamatwa pia njiani alipokuwa akielekea Tehran, ambako wakati huo alikuwa akienda kumtembelea dada yake. Ingawa uchunguzi ulibaini kuwa vijana waliohusika walifanya tukio hilo peke yao bila kuwahusisha wengine, "utawala wa hofu" ulienea, mwaka huo huo angalau wababí elfu kumi waliuawa[28].Wakati mawaziri wa serikali waliposhindana baina yao katika kuwaadhibu Wababí waliokuwa wakijulikana au wanaohisiwa, Bahá'u'lláh alikuwa miongoni mwa Wababí hawa walioadhibiwa. Akiwa maarufu kwa kuunga mkono maslahi ya dini ya Kibabí, Bahá'u'lláh alikamatwa na kuwekwa gerezani katika Siyah-Chal (shimo jeusi) chini ya ardhi ya Tehran, ambapo aliwekwa pingu nzito ambazo ziliacha makovu mwilini mwake ambayo yalidumu maisha yake yote yaliyobakia. Bahá'u'lláh alikaa gerezani katika pango hilo jeusi kwa miezi minne, ilhali mama wa Shah na maafisa wanaomuunga mkono mfalme walikuwa wakitafuta njia za kumhukumu kifo.[29]
Mwanzo wa Ufunuo
Wakati wa kipindi cha kifungo chake katika gereza la Siyah-Chal, Bahá'u'lláh huelezea juu ya matukio ya kipekee, ambapo alipokea jukumu lake la kuwa Mdhihirishaji wa Mungu, aliyeahidiwa ujio wake na Bab. Wabaha'i huona mwanzo huu wa jukumu la kiroho la Bahá'u'lláh kama mwanzo wa utimilizo wa utabiri wa Báb kuhusu "Yule ambaye Mungu atamdhihirisha".[30] Kutokana na asili ya 'kutotenganika' ya miitikio ya Bab na Bahá'u'lláh[23], Wabaha'i huona dini zote mbili kama kitengo kimoja kamili cha kidini, na ndio sababu kutangazwa kwa Bab mwaka 1844 kunachukuliwa kama tarehe ya awali ya Dini ya Kibaha'i.
Uhamisho

Wakati ilipothibitika bila shaka yoyote kwamba Bahá'u'lláh alikuwa hana hatia ya kushiriki katika jaribio dhidi ya maisha ya Shah[28], Shah hatimaye alikubali kumwachilia lakini kwa masharti kwamba Bahá'u'lláh hatimaye angehamishwa kutoka Uajemi milele.[31] Akiwa amenyimwa mali na utajiri wake mkubwa, katika msimu wa baridi kali sana wa Januari 1853, Bahá'u'lláh alisafiri kwa miezi mitatu hadi Baghdad pamoja na baadhi ya wanafamilia, maisha yake yaliyobaki yakatumika kama uhamisho katika maeneo ya Milki ya Ottoman. Safari kupitia milima mirefu katika kilele cha msimu wa baridi ilikuwa ngumu hasa kwa Bahá'u'lláh na familia yake.[32]
Wakati wa uhamisho huu, Bahá'u'lláh alihamishwa kutoka Baghdad, Iraq hadi Istanbul (Konstantinopoli), kisha Edirne (Adrianopoli) na kufika kwenye kituo cha mwisho huko Akka. Hata hivyo, upande mmoja wa uhamisho huu ulikuwa wa kijamii, ambao ulimgeuza Bahá'u'lláh kutoka kwa afisa mwenye heshima kubwa katika mahakama ya kifalme na kuwa mfungwa aliyehukumiwa na kubaguliwa.[32] Bahá'u'lláh mwenyewe alielezea dhana ya kiroho ya tukio hili kwa kusema kwamba "Uzuri Uliobarikiwa uliridhia kufungwa ili mwanadamu aweze kufunguliwa kutoka katika utumwa wake, alikubali kuwa mfungwa katika gereza hili kuu ili ulimwengu mzima upate uhuru wa kweli."[5]
Baghdad
Bahá'u'lláh alifika Baghdad Machi 1853, na baada ya kukaa kwa muda katika mji mdogo wa Qa'imayn nje ya Baghdad, alikodisha nyumba katika eneo la Karkh kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Tigris huko Baghdad.[2] Baada ya kuishi Baghdad, Bahá'u'lláh alianza kutuma mawasiliano na walimu ili kuhamasisha na kufufua ari ya wafuasi walioteswa wa Báb huko Persia. Kwa muda, Wabábi wengi walihamia Baghdad ili kuwa karibu na Bahá'u'lláh. Miongoni mwao alikuwa Mírza Yahyá, ambaye baadaye alijulikana kama Subh-i-Azal, kakaye Bahá'u'lláh wa kambo aliyekuwa mdogo kwa miaka 13, ambaye alimfuata katika dini ya Bábí, na hata alisafiri naye katika baadhi ya safari za awali. Baada ya kifo cha baba yao, elimu na malezi ya Yahyá kwa kiasi kikubwa yaliangaliwa na Bahá'u'lláh.[33] Wakati wa kifungo cha Bahá'u'lláh katika Síyáh-Chál, Yahyá alijificha, lakini baada ya Bahá'u'lláh kuhamishwa kuelekea Iraq, Yahyá aliondoka Iran kwa siri na kuingia Baghdad.[34]
Kwa muda, Yahya alifanya kazi kama katibu wa Bahá'u'lláh huko Baghdad, lakini alichochewa na wivu kutokana na kuongezeka kwa sifa za Bahá'u'lláh baina ya Wabábi, na kutamani kuongoza dini.[35][36] Akiwa anajaribu kujikuza kati ya Wabábí, Yahya na baadhi ya wafuasi wake walirejelea barua ambayo Báb aliandika miaka michache iliyopita wakati Yahya alikuwa bado kijana, ambayo ilimtaja Yahya kama kiongozi wa muda hadi atakapokuja "Yeye ambaye Mungu atamdhihirisha". Yahya alidai kwamba barua hiyo ilimaanisha kwamba kwa kweli aliteuliwa kuwa mrithi wa Báb. Wabábí wenye ufahamu walikataa haraka madai ya Yahya, kwa kuwa barua iliyorejelewa haikueleza nafasi kama hiyo, na kutokana na ukweli kwamba maandiko mengine ya Báb yalifuta wazi "taasisi ya urithi" kutoka katika dini yake.[37] Báb pia aliamuru kwamba hadi kuwasili kwa Yule Aliyesuburiwa, maneno ya mtu yeyote hayatakuwa ya lazima kwa waumini.[37] Wengine walihoji nia za Yahya, wakiona kwamba hakuwahi kufanya chochote kulinda dini ya kibábí au maisha ya Wabábí, ambayo sasa alidai nafasi ya juu.[38][39] Ili kuimarisha jaribio lake, Yahya alijaribu kumchafulia kati ya Wabábí kwa kueneza uvumi na madai ya uongo kuhusu Bahá'u'lláh, ambayo yalichochea hisia mbaya miongoni mwa Wabábí katika jamii ya Baghdad.
Bahá'u'lláh alihisi huzuni kutazama mzozo uliotokea kati ya Wabábí. Kwa kuwa mpango wowote wa Mungu hauwezi kukubaliana na hali ya kuelewana, ndiyo sababu Bahá'u'lláh aliamua kujiondoa mwenyewe kutoka hapo. Takriban mwaka mmoja baada ya kuwasili kwake Baghdad, aliondoka ghafla, bila kumwambia yeyote alikuwa anaenda wapi au jinsi ya kuwasiliana naye. Alisafiri kuelekea milima ya Kurdistan kaskazini ya Baghdad akiwa na mwenzake mmoja tu, ambako aliishi peke yake kwa mtindo wa Kisufi katika pango. Wakurdi wa eneo hilo kwa kiasi kikubwa wanatazama kwa maisha ya Kisufi kwa mwongozo wa kidini, na mmoja wa wasufi hao aligundua kuhusu Bahá'u'lláh na akaanza kuthamini hekima yake ya kiroho. Walimwalika aje katika mkutano wa Wasufi katika mji Mkuu wa Iraqi Kurdistan, Suleimaniyyah, na kuwafundisha wale wafuasi wa Kisufi waliokusanyika hapo. [40] Baadaye, katika waraka moja, aliandika kwamba hakutaka kuwa chanzo cha utofauti kati ya jamii ya Wababí. [41] [42]
Maisha Suleimaniyah na Kurejea Baghdad

Mwanzoni, wakati akiishi kama mtawa katika milima hiyo, Bahá'u'lláh alivaa kama dervish (mtawa) na alitumia jina Dervish Muhammad-i-Irani[41]. Mkuu wa semina maarufu ya kidini huko Suleimaniyah alikutana na Bahá'u'lláh[43] na akamwalika kuja. Huko, mwanafunzi mmoja aliona kazi bora ya uandishi ya Bahá'u'lláh, ambayo ilichochea udadisi wa walimu wakuu. Kwa vile aliweza kujibu maswali yao juu ya mada changamani za kidini, Bahá'u'lláh alipata sifa haraka kwa elimu na hekima yake.[44] Sheikh Uthman, Sheikh Abdurrahman, na Sheikh Ismail, viongozi wa amri za Naqshbandiyih, Qadiriyih na Khalidiyyah mtawalia, walianza kutafuta ushauri wake. Katika mojawapo ya maeneo haya, kitabu cha Bahá'u'lláh 'Mabonde Manne' kiliandikwa.[45] Kipindi cha kutokuwepo kwa Bahá'u'lláh katika jamii ya Wababi huko Baghdad kilifichua kwa uharaka hali halisi ya Mirza Yahya. Heshima ya umma na morali ya Wababi vilianguka haraka kwasababu Yahya alishindwa kutoa mwongozo wa kiroho au kuonesha viwango vya juu vya maisha vilivyofundishwa na Bab. Vitendo vyake vya kuwaaibisha Bahá'u'lláh na wale wote waliomsifu viliongezeka. Wakati huo huo, Yahya aliitumia imani ya Kibabi kwa faida ya kifedha na kuimarisha nafasi yake ya kudanganya, na kufanya mambo ambayo yalipingana na kauli za Bab kwa namna ambayo iliabisha.[46]
Polepole, kutomwamini Yahya na kutamani mwongozo wa Bahá'u'lláh kulionekana wazi miongoni mwa Wababi. Hatimaye, Wababi wa Baghdad walipata mahali alipo Bahá'u'lláh na watu wawili walifika Suleimaniyah kumchukua. Bahá'u'lláh mwanzoni hakutaka kuondoka kutoka huko Suleimaniyah. Hakika, katika miaka ya baadaye, aliandika kwamba alipoondoka Baghdad, hakuwa na nia ya kurudi tena. Hata hivyo, aliposikia kuhusu hali mbaya ya jamii ya Wababi ya Baghdad, alisema kwamba alihisi kuwa kama hakuingilia kati, dhabihu zote na ushahidi wa miaka iliyopita ya wa Wababi na Bab mwenyewe vingekuwa bure. Kwa hivyo alikubali kurudi.[32][40] Baada ya kuwa katika upweke kwa takriban miaka miwili huko Suleimaniyah, Bahá'u'lláh alirudi Baghdad tarehe 19 Machi 1856.[41]
Mara baada ya kurudi, alianza mara moja kurejesha heshima na hadhi ya jamii ya Wababi na kujenga upya ari na umoja wake. Aliandika maandiko kadhaa muhimu, kama vile kitabu chake muhimu zaidi cha Yakini, Kitáb-i-Íqán (Kitabu cha Yakini) na maandiko ya fumbo kama Mabonde Saba, Maneno ya Yaliyofichwa na mashairi kadhaa.[2] Katika miaka 7 iliyofuata, Bahá’u’lláh aliihuisha "jamii katika kiwango cha maadili na kiroho ambacho ilifikia wakati wa maisha ya Báb" kupitia mfano wa kibinafsi pamoja na msaada na mazungumzo ya kudumu na wafuasi. Watu wengi zaidi walivutiwa kujiunga na vuguvugu la Wababi lililofufuka.[41] Kuzidi kuenea kwa heshima ya Bahá’u’lláh katika Baghdad na maeneo ya jirani pamoja na kuenea kwa maandiko yao kuliwavuta "wakuu, wanazuoni, wafuasi wa mafumbo na maafisa wa serikali" kukutana nao, wengi wao walikuwa "watu mashuhuri katika maisha ya umma ya Kiajemi."[47][43] Maendeleo haya yalitia wasiwasi na kuibua upinzani miongoni mwa viongozi wa kidini wa Kiislamu wa Irani, na kwa mara nyingine yaliongeza "hofu na shaka kali" miongoni mwa mfalme wa Irani na washauri wake.[47]
Walijaribu kuandika ripoti za uwongo kuhusu Bahá'u'lláh huko Tehran na kuomba serikali ya Irani kuwa awekwe chini ya adhabu ya kifo kwa kumrudisha Irani. Hatimaye, juhudi zao zilifaulu, na serikali ya Irani rasmi iliomba serikali ya Ottoman kwamba ama Bahá'u'lláh arudishwe Irani au aondolewe Iraq ambako alikuwa karibu na mpaka wa Irani.[40]
Mwaliko wa Istanbul (Konstantinopoli) na Ufunuo wa Baháʼu'lláh
Mnamo Machi 1863, Baháʼu'lláh alipokea amri kutoka kwa serikali ya Ottoman kwenda Istanbul, mji mkuu wa Dola la Ottoman, ambapo Sultan Abdülaziz mwenyewe alimwalika Baháʼu'lláh kuishi katika mji mkuu wa Ottoman, Konstantinopoli (sasa Istanbul).[48] Mnamo Aprili 22, 1863, Baháʼu'lláh aliondoka nyumbani kwake Baghdad na kuelekea kingo za Mto Tigris na kuvuka hadi upande mwingine kuingia kwenye bustani ya kijani ya Najībīyyih, ambayo rafiki mmoja wa Baghdad alikuwa ameitoa kwa matumizi ya Baháʼu'lláh. Huko Baháʼu'lláh alikaa kwa siku kumi na mbili pamoja na wanafamilia na baadhi ya wafuasi wake wa karibu waliochaguliwa kuandamana naye. Alipowasili bustanini, Baháʼu'lláh aliwatangaza kwa wenzake kwamba yeye ni "Yule ambaye Mungu atamdhihirisha," kama alivyoahidi Bab,[49], na kutangaza kwamba dhamira yake kama Mdhihirishaji mpya wa Mungu duniani imeanza.[43][50] Kipindi hicho cha siku kumi na mbili, ambapo Baháʼu'lláh alijitangaza kuwa ndiye Mtume aliyetabiriwa na Bab, kinaadhimishwa kila mwaka na Wabaha'i na huitwa Sikukuu ya Ridván, Mfalme wa Sherehe. [32]
Bahá'u'lláh aliondoka kwenye Bustani ya Ridván tarehe 3 Mei 1863 na kusafiri na familia yake kwenda Constantinople kama wageni wa serikali ya Ottoman wakiwa na ulinzi wa serikali ya wapanda farasi iliyopangwa na waziri mkuu wa Sultan, 'Ali Pasha', kwa ajili ya usalama wao.[51] Wasafiri wengine kadhaa waliomba ruhusa kutoka kwa Bahá'u'lláh ili kuongozana nao. Ingawa Mirza Yahya hakuwepo katika mwaliko wa Sultan, alijiunga na kundi hilo njiani.[52] Baada ya majuma kumi na tano, Bahá'u'lláh alifika kwenye mji mkuu wa Ottoman tarehe 16 Agosti 1863. Alipokelewa na mawaziri mbalimbali wa serikali ya Sultan na watu mashuhuri waliompa heshima ya kukutana nae. Balozi wa Kiajemi pia alituma mabalozi kumkaribisha siku iliyofuata ya kuwasili kwake.[53]
Bahá'u'lláh alikaa Istanbul kwa miezi mitatu. Katika kipindi hiki, alikataa kuomba msaada kutoka kwa mawaziri wa serikali au kukutana na Sultan, ambayo ilikuwa ni taratibu ya kawaida kwa watu mashuhuri waliowasili Istanbul. Alisema kuwa aliitwa Istanbul na serikali ya Ottoman na hakuwa na tamanio lolote la kuomba au kuhamasisha mpango wowote. Ukosefu wa urafiki na hali ya Bahá'u'lláh ilitumiwa vibaya na balozi wa Uajemi ambapo alimwasilisha Bahá'u'lláh vibaya kwa kudhamiria mbele ya mahakama ya Ottoman[54] na kushinikiza kufukuzwa kwake kutoka mji mkuu[55]. Matokeo yake, mwishoni mwa kipindi hiki, amri ilitolewa kwamba Bahá'u'lláh afukuzwe hadi Edirne, mji mkuu wa mkoa, ambao sasa upo katika Uturuki ya Ulaya, na Sultan alikubali bila kusita. [40]
Uhamisho wa Adrianople
Tarehe 12 Desemba 1863, Bahá'u'lláh alifika Adrianople pamoja na familia yake na wafuasi wengine. Uwepo wake huko, ambao uliendelea kwa miaka minne na nusu, ulikuwa kipindi muhimu katika kuendeleza zaidi jukumu lake miongoni mwa Wababi na kutangaza lengo lake kwa ujumla.[56] Katika miaka miwili iliyofuata, maandiko yaliyotoka kwa Bahá'u'lláh yalienea kwa Wababi nchini Iran. Bahá'u'lláh alituma wafuasi kadhaa waaminifu Iran, na wengi wa Wababi walianza kumtambua kama kiongozi wa imani yao.[57][58]
[52] Akiwa amechochewa na ukosefu wa mateso dhidi ya Wababi, Mirza Yahya aliamua "kujitokeza kutoka katika upweke aliouweka mwenyewe" ili kufufua matarajio yake ya uongozi, ambayo yalisukumwa na wivu wake dhidi ya Baha'u'llah. Akiamini kwamba kifo cha Baha'u'llah kilikuwa muhimu kwa ajili ya kutimiza dhamira yake, jaribio la kwanza la Yahya katika mwelekeo huu lilikuwa ni jaribio la kumtilia sumu Baha'u'llah alipomwalika kwenye chai. [59][60] Hii ilisababisha Baha'u'llah kuugua vibaya kwa karibu mwezi mmoja, na kubakia na madhara ya kuwa na mikono inayotetemeka kwa maisha yake yote yaliyobakia. Ingawa Baha'u'llah aliwaambia wale waliojua kinachoendelea wasizungumze kuhusu tukio hilo, ufahamu wa tukio hilo ulienea, ukisababisha machafuko makubwa kati ya Wababi. Hata hivyo, lilikuwa jaribio la baadaye la Yahya kwenye maisha ya Baha'u'llah lililosababisha "vurugu kubwa katika jamii."[61] Hili lilihusisha Ustadh Muhammad-Ali-i-Salmani, ambaye alikuwa kinyozi wa jadi aliyekuwa akihudumia Baha'u'llah katika bafu lake.[52] Salmani alieleza kuwa Yahya alianza ghafla kumwonesha urafiki, kisha siku moja akasisitiza kwamba itakuwa "huduma kubwa kwa dini yao" ikiwa atamuua Baha'u'llah wanapokuwa katika bafu. Salmani alichukizwa na wazo hili kiasi kwamba alikiri kwamba wazo lake la kwanza lilikuwa kumuua Yahya—alijizuia tu kwa sababu alijua kuwa kufanya hivyo kungemkasirisha Baha'u'llah. Katika hasira yake alisimulia juu ya tukio hilo kwa Mirza Musa, kaka mwaminifu wa Baha'u'llah, ambaye alimsihi kulipuuza, akisema Yahya alikuwa amelifikiria kwa miaka. [62] Akiwa bado na wasiwasi, Salmani alieleza suala hilo kwa mwana mkubwa wa Baha'u'llah, Abdu'l-Baha, na kuambiwa asiwaambie wengine. Hatimaye Salmani alimjulisha Baha'u'llah, ambaye pia alimwambia asizungumzie jambo hilo na mtu yeyote. Hadi tukio hili, kwa sababu Yahya alikuwa kaka wa kambo ambaye Baha'u'llah alikuwa akimhudumia kwa huruma na fadhili, Wababi wengi walimheshimu Yahya, lakini Salmani alipokosa ukimya na kuwaambia wengine waziwazi kile alichomuombwa na Yahya kufanya [63], matendo na nia za Yahya, ambazo zilikuwa kinyume na mafundisho ya Bab, zilibua machafuko makubwa kati ya Wababi.[64]
Uhamishoni wa Mwisho huko Akka

Baada ya kupoteza heshima au ushawishi kati ya Wafuasi wa Bab waliokuwa wameikubali dini ya Kibahá'í, Mírzá Yaḥyá alijaribu tena kumchafua Bahá'u'lláh mbele ya maafisa wa Ottoman, akimshutumu kwa kupanga njama dhidi ya serikali ya Kituruki.[65][66] Vitendo vya Yaḥyá vilichochea uchunguzi wa serikali, ambao baada ya uchunguzi ulimwachilia Bahá'u'lláh, lakini kwa hofu ya masuala ya kidini kuleta machafuko siku za usoni, serikali ya Ottoman iliamua kuwafunga Bahá'u'lláh na Mírzá Yaḥyá katika vituo vya mbali vya miliki yao.[67][65] Mwezi Julai 1868, amri ya kifalme ilimtia hatiani Bahá'u'lláh na familia yake kwa uhamisho wa kudumu kwenye koloni la adhabu la magonjwa huko Akka; wengi wa Wafuasi wa Kibahá'í walihamishwa kutoka Adrianople pamoja nao.[68] Kutokana na njama zake mwenyewe, Mírzá Yaḥyá, aliwekwa pia gerezani - kwa sababu maafisa wa Kituruki walishuku kuwa alikuwa na njama fulani, alifungwa gerezani huko Famagusta, Cyprus pamoja na familia yake, baadhi ya wafuasi wake, na wafuasi wanne wa Kibahá'í.[69][70][71]

Bahá'u'lláh na wenzake waliondoka Adrianople tarehe 12 Agosti 1868, na kufika Akka tarehe 31 Agosti ambako walifungwa gerezani ndani ya mji.[65] Wakazi wa Akka waliambiwa kuwa wafungwa wapya walikuwa ni maadui wa ufalme, Mungu na dini yake, na walikatazwa vikali kuwa na uhusiano wowote nao. Miaka ya awali huko 'Akka' ilikuwa na mazingira magumu sana na wengi wa Wafuasi wa Bahá'í waliugua (hatimaye watatu walifariki).[65] Mwezi Juni 1870, Mírzá Mihdí, mwana wa Bahá'u'lláh mwenye umri wa miaka 22, alikufa kwa huzuni, alipokuwa akisali na kutafakari jioni wakati alipoanguka kutoka kwenye paa la jengo gerezani ambako hakukuwa na uangalizi wa kutosha.[72][73] Baadaye, mahusiano kati ya wafungwa wa Kibahá'í, maafisa, na jamii ya ndani yaliboreshwa, na hivyo masharti ya ufungwaji wao yalilegezwa. Mwezi Aprili 1871, wakati alipotembelea Akka, Dkt. Thomas Chaplin (mkurugenzi wa hospitali inayoendeshwa na Uingereza huko Yerusalemu) alikutana na ʿAbdu'l-Bahá kwa niaba ya Bahá'u'lláh katika nyumba ambako familia yake iliishi baada ya kuondoka gerezani. Baadaye, daktari huyo aliandika barua kwa mhariri wa gazeti la The Times kuhusu Bahá'u'lláh, iliyochapishwa tarehe 5 Oktoba 1871.[74] Hatimaye, baada ya kifo cha Sultani, Bahá'u'lláh alipewa ruhusa ya kuondoka mjini kutembelea sehemu za jirani, na kisha kuishi katika maeneo nje ya Akka. Mwaka 1873, matukio mawili muhimu yalitokea; kwanza, Bahá'u'lláh alikamilisha kitabu chake muhimu zaidi, Kitáb-i-Aqdas (Kitabu Kitakatifu Kabisa), ambacho kina sheria za dini mpya pamoja na maelekezo ya maadili na kijamii pamoja na masuala ya utawala. Pili, ʿAbdu'l-Bahá na Munīriyya Khānum, binti ambaye alitoka katika familia ya Mbahá'í mashuhuri huko Isfahan, walifunga ndoa. Mwaka 1876, ʿAbdu'l-Bahá alifanya mipango kwa ajili ya Bahá'u'lláh kuenda nje ya mipaka ya mji, akianza na kutembelea bustani (inayojulikana kama Bustani la Riḍwán) iliyolipiwa kodi na ʿAbdu'l-Bahá. [32][40] Kuanzia 1877 hadi 1879, Bahá'u'lláh aliishi katika nyumba yenye umbali wa maili chache kaskazini mwa mji wa magereza, huko Mazra'ih.[75] Hata hivyo, akiwa rasmi bado ni mfungwa wa Dola ya Ottoman, miaka ya mwisho ya maisha ya Bahá'u'lláh (1879-1892) yalitumika katika jumba la Bahjí lililo nje tu ya Akka. Bahá'u'lláh alitumia muda wake kuandika vitabu kadhaa vinavyoeleza mafundisho yake, ikiwa ni pamoja na dhana ya dunia iliyounganika, haja ya vitendo vya maadili na sala nyingi.
Mnamo mwaka 1890, msomi wa Kiorientali wa Cambridge, Edward Granville Browne alifanikiwa kufanya mahojiano na Bahá'u'lláh huko Bahjí. Baada ya kukutana naye, aliandika taswira maarufu ya maelezo ya Bahá'u'lláh:
Katika kona ile, karibu na ukuta, alikaa mtu wa ajabu na mwenye heshima... Sitaweza kamwe kuusahau uso ambao macho yangu yaliuona, ingawa siwezi kuuelezea. Macho yake yanayopenyeza yanaweza kusoma nafsi ya mtu; nguvu na mamlaka vilikaa juu ya paji la uso mkubwa; huku mapaji ya uso na uso wenye mistari mizito ikionyesha ishara ya umri.. Haikuhitajika kuuliza nilikuwa mbele ya nani, kwani nilijiinamishia mbele ya chanzo cha ibada na upendo ambao wafalme wanaweza kumuonea gere na watawala wanaweza kusikitika bure! Sauti laini, yenye heshima ilinialika kuketi, kisha ikaendelea: - "Sifa iwe kwa Mungu kwamba umefanikiwa kufika!…Umekuja kumuona mfungwa na mhamishwa…Tunatamani tu mambo mema ya ulimwengu na furaha ya mataifa; walakini wao wanadhania sisi ni wachochezi wa ugomvi na maasi tustahilio kifungo na uhamisho…Kwamba mataifa yote yawe taifa moja katika imani na watu wote kama ndugu; kwamba mafundo ya huba na umoja miongoni mwa watoto wa watu yaimarishwe; kwamba tofauti za kidini zikome, na tofauti za kimbari zifutwe—kuna madhara gani katika hili? … Walakini hivyo ndivyo itakavyokuwa; ugomvi huu usio na manufaa; vita hivi viharibifu vitakwisha, na ‘Amani Kuu Kabisa’ itakuja…Je, ninyi huko Ulaya hamhitaji hili pia? Siyo hiki ambacho Kristo alikitabiri?…Walakini tunawaona wafalme na watawala wenu wakifuja hazina zao kwa wingi na kwa uhuru zaidi kwenye mambo yanayoangamiza jamii ya wanadamu kuliko yale ambayo yangesaidia kuleta furaha ya jamii ya wanadamu.…ugomvi huu na umwagaji huu wa damu na mafarakano sharti vikome, na watu wote wawe kama ukoo mmoja na familia moja.… Acha mtu asijitukuze katika hili, kwamba huipenda nchi yake; bali mwache ajitukuze katika hili, kwamba huipenda aina yake…"[76][77]
Bahá'u'lláh alitumia miaka yake ya mwisho ya maisha yake huko Bahji, ambapo aliongoza kazi zake na kukutana na idadi inayoongezeka ya wahujaji wa Kibahá'í na Wabahá'í waliokuwa wakiishi katika eneo hilo. Bahá'u'lláh alifariki tarehe 29 Mei 1892 baada ya ugonjwa wa muda mfupi.[2] Alizikwa katika jengo lililokuwepo karibu na kasri la Bahji ambalo sasa linajulikana kama kaburi lake.[78] Ni mahali pa hija na mahali patakatifu zaidi kwa Wabahá'í duniani kote[79], na ni Qiblah wanayogeukia kwa sala za lazima za kila siku.[80] Mnamo 2008, kaburi la Bahá'u'lláh liliongezwa kwenye orodha ya maeneo ya Urithi wa Dunia ya UNESCO pamoja na maeneo mengine matakatifu ya Kibahá'í huko Akka na Haifa.[81]
Mafundisho
Mungu
Dhana ya Mungu katika imani ya Kibaha'i ni ya umoja wa Mungu mmoja. Mungu ni asili isiyoumbika na isiyoharibika ambayo ndio chanzo kamili na cha mwisho cha uwepo wote.[82][83] Bahá'u'lláh anafundisha wazi "uwepo na umoja wa Mungu, kuwa chanzo kisichojulikana, kisichoweza kufikiwa, cha ufunuo wote wa siri, wa milele, mwenye kujua yote, mwenye kuwa kila mahali na mwenye nguvu zote."[84] Bahá'u'lláh alisisitiza kuwa Muumba hawezi kueleweka na viumbe - kwa sababu kiumbe chochote hakiwezi kumuelewa Muumbaji wake.[85] Hata hivyo, Bahá'u'lláh alisema kuwa Muumba amempa binadamu uwezo wa kutambua uwepo wake, na uwezo wa kukua kiroho kwa kuzielewa sifa nzuri zisizo na kikomo za Mungu na kufanya jitahida kuonesha sifa hizo kadiri wanavyoweza katika maisha yao[86][87] - kama vile upendo, huruma, wema, ukarimu, haki, na kadhalika.
Wajumbe wa Mungu
Bahá'u'lláh anaeleza kuwa maarifa ya Mungu na sifa za Muumba kwa wanadamu zinaweza kufahamika tu kupitia Wajumbe wa Mungu wa enzi hiyo. Tofauti na njia hiyo, haiwezekani kwa ulimwengu wa kibinadamu. Bahá'u'lláh na Báb wote wawili wameelezea kuhusu wajumbe wa Mungu.[88] [89] Badala ya kuwa waangalizi wakuu wenye mawazo bora katika maisha ukilinganisha na wengine, wajumbe wa Mungu ni viumbe vya kiroho walioumbwa mahsusi na Mungu, ambao uwezo wao unazidi ule wa wanadamu wa kawaida kwa kiasi kisicho na kipimo. Kabla ya kuzaliwa katika maisha haya ya kidunia, kila Mjumbe wa Mungu alikuwepo katika ufalme wa kiroho, na hutumwa na Mungu katika kipindi maalum na mahali kama chombo cha mwongozo wa kiungu ili kusaidia binadamu kuelewa na kuendeleza uwezo wao wa ndani polepole, ili kutimiza mpango wa Mungu.[90]
Wabahá'í wanaamini kwamba hizi dhihirisho za kimungu zinaonesha mwanga wa mapenzi na madhumuni ya Mungu katika dunia hii. Maandishi ya Kibahá'í yamelinganisha Mitume na vioo kamili vinavyoakisi jua - ingawa kila kioo ni tofauti, bado kila mwangaza unaotolewa ni wa jua lilelile, na tu tofauti zinatokana na wakati na hali.[91] Bahá'u'lláh anasema kwamba mwongozo wa Mitume unatofautiana kiasili kutokana na hali na mahitaji maalum ya wale wanaoshughulika nao:
"Wachukuzi wa ujumbe wa Mungu wanapaswa kuzingatiwa kama waganga ambao kazi yao ni kukuza ustawi wa dunia na watu wake... basi haishangazi kwamba matibabu yaliyowekwa na daktari katika siku hii yanatofautiana na matibabu yaliyowekwa katika nyakati zilizopita. Inakuaje vinginevyo wakati mgonjwa huhitaji matibabu maalum kwa kila hatua ya mwendo wa ugonjwa unaomuathiri? Kila mara Mitume wa Mungu wameipa dunia mwangaza wa siku moja kali zaidi. Kwa njia hiyo hiyo, kila mara Mitume wa Mungu walipoangaza dunia kwa mwanga wa ajabu wa jua ya ufahamu wa kimungu, wamewaita watu wao kuchukua mwanga wa Mungu kupitia njia zinazofaa zaidi za mahitaji ya zama ambazo walidhihirika ndani yake.[92][93]
Wabahá'í wanaona kila dini kubwa duniani kama sehemu ya mchakato wa kijumla wa kielimu ulioamriwa na Mungu[94] ambao umewezesha ustaarabu wa binadamu kusonga mbele kiroho na kijamii - ambapo watu wamejifunza kukumbatia muunganiko unaokua wa umoja, ambao hatimaye umejumuisha familia zinazozidi kuwa nyingi zaidi, hadi kabila, hadi eneo, na kisha taifa. Hatimaye, wanadamu itabidi wakumbatie mzunguko wao wa mwisho wa umoja, yaani dunia yote.[95]
Kanuni za Kijamii
Bahá'u'lláh daima alisema kwamba ujumbe wake ni kwa ajili ya watu wote, na mafundisho yake yanalenga kujenga dunia mpya ambapo jamii ya binadamu itaendelea kwa umoja na kwa pamoja. Anatangaza waziwazi kanuni ya umoja wa binadamu[7], akiwashauri viongozi wa mataifa kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya sasa ili kufikia amani na kuimarisha ulinzi huo kupitia usalama wa pamoja.[96] Ili kuhimiza maendeleo ya jamii ya dunia iliyoungana, Bahá'u'lláh anasisitiza umuhimu wa kuondoa ubaguzi wa kidini na wa kikabila na kuepuka utaifa uliokithiri.[97] Zaidi ya hayo, anasema kwamba haki za wachache zinapaswa kulindwa na maendeleo yao yahimizwe.[98] Masharti yanayohitajika kwa ajili ya kufikia amani ya kimataifa ni usawa kamili kati ya wanawake na wanaume kote duniani.[99] Bahá'u'lláh anasema kwamba machoni pa Mungu, wanawake na wanaume ni sawa; hakuna anayemzidi mwenzake.[100] Ili kufanikisha usawa huo, mafundisho ya Bahá'i yanapendekeza kutekelezwa kwa mabadiliko makubwa ya kijamii kila mahali[101], ikihusisha kuondolewa kwa mazoea ya kibaguzi dhidi ya wanawake na kutilia mkazo zaidi elimu kwa wasichana[102] ili kuhakikisha kwamba wanawake wanaweza kutimiza uwezo wao katika nyanja zote za jitihada za kibinadamu.[103]
Urithi na Agano lake

Bahá'u'lláh aliweka agano wa wazi na Wabahá'í katika wosia na barua yake ya tamaa, ambayo iliandikwa kabisa kwa mkono wake mwenyewe na inajulikana kama "Kitabu cha Agano". Siku ya tisa baada ya kifo chake mwaka 1892, ilisomwa mbele ya mashahidi na wanachama wa familia yake.[104] Ili kutoa kitovu cha mwongozo endelevu, kinachoweza kufafanua na kufasiri maandiko yake inapohitajika, Bahá'u'lláh alikabidhi uongozi huo kwa mwanawe mkubwa Abdu'l-Bahá katika wosia wake. Yeye ndiye mrithi wa dini ya Kibahá'í, mfasiri pekee aliyeidhinishwa wa maandiko yake, mfano wa mafundisho yake, na kitovu cha agano lake kwa Wabahá'í wote.[105][106][107] Uteuzi wa wazi wa Abdu'l-Bahá ulikubaliwa kwa urahisi na Wabahá'í wengi kama tukio lililotarajiwa, kwani kwa miongo kadhaa kabla ya kifo cha Bahá'u'lláh, Abdu'l-Bahá alijulikana kwa kutekeleza majukumu aliyopatiwa na Bahá'u'lláh kwa namna yenye uwezo mkubwa na kujitolea.[108][109]
Bahá'u'lláh aliunda muundo wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, taasisi yenye wajumbe tisa ambao wangeweza kutunga sheria juu ya masuala ya kiimani, na alielezea jukumu la kuteuliwa kwa vizazi vyake, ambayo yote yalielezwa kwa mapana na ʻAbdu'l-Bahá alipo mteua Shoghi Effendi kama mlinzi. Nyumba ya Haki ya Ulimwengu iliyochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1963, ni chombo kikuu cha usimamizi cha jamii ya Kibahá'í duniani kote. Mtu yeyote anayekataa kiungo chochote katika mfululizo huu wa uongozi anachukuliwa kama mvunjaji wa agano.[110]
Nguvu ya Agano kwa Wabahá'í na ahadi ya umoja iliyoanzishwa na Bahá'u'lláh inalinda dini yao dhidi ya mgawanyiko na utofauti, tatizo ambalo limeathiri dini za huko nyuma. Kupitia Agano, dini ya Kibahá'í imezuia migogoro, na jitihada mbalimbali za kuanzisha uongozi mbadala zimekosa mvuto mkubwa kwa wafuasi kutokana na ukosefu wa mamlaka ya kiimani.[110]
Utawala wa Kibaha'i

Katika nchi nyingi, masuala ya jamii za Kibaha'i yanasimamiwa kwa kutumia kanuni za ushauriano[111] na maamuzi ya pamoja[112]. Kwa kuwa katika dini la Kibaha'i hakuna makasisi, hakuna mbaha'i mwenye haki ya kumwambia mwingine jinsi anavyopaswa kufikiri au kufanya.[113] Bahá'u'lláh aliwahimiza sana wabaha'i kushiriki mafundisho yake lakini alikataza ubadilishaji kwa nguvu.[114] Kufanya kazi katika vikundi na ushiriki katika shughuli za kijamii huchukuliwa kama vipengele muhimu vya maisha ya Kibaha'i.[115] Ikitakiwa au inapohitajika, juhudi za mtu mmoja mmoja na za kikundi na kwa ujumla shughuli za jamii ya kibaha'i huratibiwa, kuelekezwa na kuungwa mkono na mabaraza ya watu tisa (yanayochaguliwa kila mwaka kwa kupiga kura za siri) yanayofanya kazi katika ngazi za eneo, kanda na kitaifa.[116] Utiaji moyo wa ziada na mwongozo wa kiroho hutolewa na watu walioteuliwa ambao hawana mamlaka ya utekelezaji.[117][118] Miradi ya kibaha'i inaungwa mkono kikamilifu na hazina inayotolewa kwa hiari na Kibaha'i wenyewe, kwani dini ya kibaha'i haikubali michango kutoka kwa watu ambao si waumini wake wamejitangaza.[119] Wajumbe wa asasi yoyote ya Kibaha'i, pamoja na mtu yeyote aliyeteuliwa nao kusaidia katika shughuli mbali mbali za jamii (kama vile madarasa ya mafunzo ya kimaadili kwa watoto na vijana chipukizi), wanahudumu kwa hiari. Utaratibu wa kiutawala wa Kibaha'i unaongozwa na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu[120], asasi hii iliteuliwa na kuthibitishwa na Bahá'u'lláh katika kitabu chake cha sheria kwa ajili ya kusudi hili hilo; Nyumba ya Haki ya Ulimwengu huchaguliwa kila miaka mitano katika mkutano wa kimataifa unaoandaliwa katika Kituo cha Ulimwengu cha Kibaha'i na wawakilishi wa Wabaha'i kutoka dunia nzima.[121][122][123]
Maandishi ya Bahá'u'lláh
Asili

Wabahá'í wanaamini kwamba maandiko yote ya Bahá'u'lláh yalifunuliwa kwa njia ya kiungu, hata yale yaliyoandikwa kabla ya kujitangaza kuwa yeye ni mjumbe wa Mungu.[110][124] Wakati Bahá'u'lláh alipokea ufunuo, mara nyingine aliandika mwenyewe, lakini mara nyingi alitamka maneno kwa sauti mbele ya mwandishi wa maandiko. Wakati mwingine alikuwa anaongea kwa kasi sana kiasi kwamba iliwasumbua wale waliokuwa wanarekodi maneno yake.[125] Maandishi mengi ya Bahá'u'lláh yameandikwa kama barua fupi au risala zilizolengwa kwa mtu mmoja au zaidi.[110] Miongoni mwa kazi zake kubwa ni Maneno Yaliyofichwa, Mabonde Saba, Kitabu cha Yakini(Kitáb-i-Íqán), Kitáb-i-Aqdas (Kitabu Kitakatifu Kabisa), na Barua kwa Mwana wa Mbwa Mwitu. Maandiko ya Bahá'u'lláh yameandikwa awali katika Kifarsi na Kiarabu. Maandiko yake ni sawa na zaidi ya vitabu 100 - karibu kazi zake 15,000 zimepatikana na kuthibitishwa.[126]
Yaliyomo
Mada za maandiko yake ni pana na zinaongelea maudhui yanayohusiana na maisha ya binadamu, kanuni za kijamii, kimaadili na kiroho kwa watu binafsi na makundi. [127] Vipengele hivi vinajumuisha maoni kuhusu maandiko, unabii na imani za dini zilizotangulia; [128] kufuta sheria za awali, na kuanzisha sheria na amri za mpango huu mpya; [129] maandiko ya mafumbo; [130] madai na maelezo yanayodaiwa kuhusu Mungu; matamko yanayohusiana na uumbaji wa roho ya binadamu kuwa asili kuu ya Mungu, [131] ambayo ina uwezo wa kujua kwamba Muumba yupo na roho ya binadamu ina uwezo wa kuakisi sifa zote za Mungu; madai ya uwepo wa maisha baada ya kifo na maelezo kuhusu jinsi roho zinavyoendelea kwa milele katika malimwengu wa kimungu yasio na kipimo [132][133]; kuinua kazi inachofanywa kwa roho ya huduma hadi hadhi ya ibada; maelezo juu ya utawala wa haki na kujenga umoja na utaratibu wa dunia; ufafanuzi juu ya maarifa, falsafa, alkemia, tiba na maisha yenye afya; kanuni za kiroho zilizounganishwa katika mafundisho ya kijamii; wito wa elimu ya wote; na kuishi kwa wema na kulingana na mapenzi ya Mungu. Bahá'u'lláh pia huchunguza teolojia na sababu za magumu katika maisha haya [134]; na ameandika maombi na maandiko mengi kwa ajili ya tafakari. [135][136]
Barua kwa Viongozi wa Dunia
Bahá'u'lláh aliandika mfululizo wa barua akiwalenga wafalme, viongozi wa kisiasa, na viongozi wa kidini, mmoja mmoja na kwa pamoja, akidai kwamba alikuwa mtu aliyeahidiwa katika Taurati, Injili, na Kurani. Aliwaomba wakubali ufunuo wake, waachane na mali zao za kidunia, watawale kwa haki, walinde haki za watu wasiokuwa na uwezo, wapunguze silaha zao, watatue tofauti zao, na kufanya juhudi kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa dunia na umoja wa watu wake. Aliwaonya kwamba dunia ya wakati huo ilikuwa karibu kufikia mwisho wake na ustaarabu wa kimataifa ulikuwa unazaliwa. Bahá'u'lláh alieleza zaidi kwamba nguvu kali za kihistoria ziko kazini na viongozi wanapaswa kutumia mamlaka waliyopewa na Mungu ili kuhudumia binadamu na kuleta haki, amani, na umoja.[137]
[138] Ujumbe wa kwanza ulikuwa umeandikwa kwa Sultan Abdul-Aziz wa Ufalme wa Ottoman huko Konstantinopoli baada ya Bahá'u'lláh kuamriwa kuhamishwa hadi Adrianopoli mwaka 1863; ujumbe mwingine uliandikwa huko Adrianopoli na 'Akká[139]. Jumla, ziliwaelekezwa kwa: Tsar Alexander wa pili wa Urusi; Francis Joseph wa Kwanza wa Austria-Hungary; Napoleon III wa Ufaransa; Naser al-Din Shah wa Uajemi; Pope Pius IX; na Malkia Victoria wa Uingereza na Ireland; Sultan Abdul-Aziz wa Kituruki; Wilhelm wa Kwanza wa Prussia; watawala na marais wa jamhuri za Marekani; wawakilishi waliochaguliwa wa watu katika kila nchi; na viongozi wa dini[140]. Ingawa walioandikiwa waliripotiwa hawakujibu kwa kiasi kikubwa, baadaye barua za Bahá'u'lláh zilivutia sana kwa "utimilifu usio wa kawaida wa unabii wake binafsi," zikimwonya Napoleon, Papa, na Kaiser (na hatimaye watu wengine maarufu pia) kuhusu matokeo ya kutotii au kufanya makosa. Wilhelm, Tsar, Emperor Francis Joseph, Shah, Sultan, na mawaziri wao wakuu na mawaziri wa kigeni waliopoteza mamlaka, maeneo, au kukutana na adhabu zingine za kimungu kwa kutotii ushauri[141][142].
Mwandishi maarufu Christopher de Bologne aliandika
Baha'u'llah hakufanikiwa kuwavuta viongozi wa enzi zile kuelekea upande wake, ambao aliwaandikia barua, au 'nyaraka', na kuwataka wakabidhi falme zao mbele yake. Malkia Victoria alijibu kwa kujikwamua; Tsar aliahidi kuchunguza zaidi. Napoleon wa Tatu alichana barua hiyo na kusema kwamba ikiwa Baha'u'llah ni Mungu, basi yeye pia ni Mungu. Nasir al-Din Shah alimwua mjumbe wa Baha'u'llah.
Uhifadhi na Tafsiri
Kituo cha Ulimwengu cha Kibaha'i kinafanya juhudi endelevu kuhakikisha kuwa maandiko asili ya Baha'u'llah yanakusanywa, yanathibitishwa, yanasajiliwa na yanahifadhiwa.[143][144] Kupitia mpango wa kimataifa wa tafsiri unaoendelea, maandiko ya Baha'u'llah yanapatikana katika lugha zaidi ya 800 kwa sasa.[145]
Maelezo
- ↑ Smith 2000, p. xiv–xv, 69–70.
- 1 2 3 4 5 6 Stockman, Robert H. (2022). The world of the Bahá'í faith. Routledge worlds series. London New York (N.Y.): Routledge, Taylor & Francis Group. ku. 38–39. ISBN 978-1-138-36772-2.
- 1 2 Hartz 2009, p. 38.
- ↑ Smith 2000, p. 323.
- 1 2 arise to serve. Cali, Columbia: Ruhi Institute. 1987. uk. 46. ISBN 9789585988095.
- ↑ Stockman 2013, p. 2.
- 1 2 Stockman 2022a, p. 219–220.
- 1 2 Smith 2000, p. 13.
- ↑ Adamson 2007, p. 267.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 127n.
- 1 2 Momen 2022, p. 41.
- ↑ Dehghani 2022, p. 188–189.
- ↑ Smith 2000, p. 58–59.
- ↑ Taherzadeh 1992, p. 34–38.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 35–37.
- ↑ Momen 2019a.
- ↑ Smith 2000, p. 73.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 30.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 9–18.
- ↑ Smith 2000, p. 57.
- ↑ Mahmoudi 2022, p. 384–387.
- ↑ Saiedi 2008, p. 343.
- 1 2 Saiedi 2008, p. 344.
- ↑ Effendi 1944, p. 23.
- ↑ Saiedi 2000, p. 295.
- ↑ Hartz 2009, p. 32.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 20–21.
- 1 2 Saiedi 2000, p. 4.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 99–101.
- ↑ BBC 2009.
- ↑ Adamson 2007, p. lxxiv.
- 1 2 3 4 5 Momen, Moojan (2007). Baha'u'llah: a short biography. A Oneworld book. Oxford: Oneworld. ku. 114-117. ISBN 978-1-85168-469-4.
- ↑ Smith 2000, p. 53.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 34.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 34–46.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 113–114.
- 1 2 Saiedi 2008, p. 344–345.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 113.
- ↑ Schaefer, Towfigh & Gollmer 2000, p. 534–535.
- 1 2 3 4 5 Balyuzi, H. M. (1980). Baha'u'lláh. 1 (tol. la Reprint). Oxford: Ronald. ku. 339-353. ISBN 978-0-85398-090-2.
- 1 2 3 4 Smith 2008, p. 17.
- ↑ Saiedi 2000, p. 117.
- 1 2 3 Momen 2022, p. 44.
- ↑ Smith 2000, p. 74.
- ↑ Smith 2000, p. 159.
- ↑ Saiedi 2000, p. 206.
- 1 2 Hatcher & Martin 1984, p. 37.
- ↑ Taherzadeh 2000, p. 68–69.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 37–38.
- ↑ Adamson 2007, p. 409–410.
- ↑ Taherzadeh 2000, p. 69.
- 1 2 3 Momen 2022, p. 44–45.
- ↑ Taherzadeh 2000, p. 75–76.
- ↑ Taherzadeh 1977, p. 1.
- ↑ Hartz 2009, p. 47.
- ↑ Hartz 2009, p. 141–142.
- ↑ Taherzadeh 1977, p. 75–77.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 38–39.
- ↑ Smith 2008, p. 24.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 225.
- ↑ Taherzadeh 2000, p. 117.
- ↑ Balyuzi 2000, p. 229.
- ↑ Salmání 1982, p. 51–52.
- ↑ Taherzadeh 2000, p. 117–120.
- 1 2 3 4 Smith 2008, p. 26.
- ↑ Hartz 2009, p. 49–50.
- ↑ Adamson 2007, p. 326–327.
- ↑ Alkan 2022, p. 76.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 42.
- ↑ Warburg 2006, p. 177.
- ↑ Nakhjavani 1983, p. vii+.
- ↑ Momen 2022, p. 47.
- ↑ Adamson 2007, p. 322.
- ↑ Momen 1981, p. 209–212.
- ↑ Smith 2008, p. 26–27.
- ↑ Momen 1981, p. 229–230.
- ↑ Smith 2008, p. 27.
- ↑ Adamson 2007, p. 59.
- ↑ Warburg 2006, p. 450–454.
- ↑ Smith 2008, p. 162.
- ↑ UNESCO World Heritage Centre 2008.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 74.
- ↑ Warburg 2006, p. 12.
- ↑ Matthews 2005, p. 19.
- ↑ Bolodo-Taefi 2022, p. 176–178.
- ↑ Kluge 2022, p. 230–231.
- ↑ Smith 2008, p. 117–118.
- ↑ Bolodo-Taefi 2022, p. 182–184.
- ↑ Adamson 2007, p. 186–188.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 120.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 116–118.
- ↑ Baháʼu'lláh 1976, p. 80, §XXXIV.
- ↑ Dehghani 2022, p. 190.
- ↑ Smith 2000, p. 246–247.
- ↑ Smith 2000, p. 323–324.
- ↑ Mahmoudi 2022, p. 390–391.
- ↑ Smith 2008, p. 53, 139.
- ↑ Hartz 2009, p. 111–112.
- ↑ Pearson 2022, p. 250–251.
- ↑ Smith 2008, p. 143–144.
- ↑ Pearson 2022, p. 251–252.
- ↑ Smith 2000, p. 131.
- ↑ Smith 2008, p. 41.
- ↑ Smith 2000, p. 114.
- ↑ Alkan 2022, p. 72.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 50.
- ↑ Momen 2004, p. 97–98.
- ↑ Alkan 2022, p. 78–79.
- ↑ Smith 2008, p. 43.
- 1 2 3 4 Smith 2000.
- ↑ Smith & Ghaemmaghami 2022b, p. 454–460.
- ↑ Warburg 2006, p. 196.
- ↑ Hartz 2009, p. 113.
- ↑ Hartz 2009, p. 118–121.
- ↑ Hartz 2009, p. 101–102, 113.
- ↑ Smith 2008, p. 178–180.
- ↑ Smith 2000, p. 276.
- ↑ Warburg 2006, p. 209–210.
- ↑ Warburg 2006, p. 306–308.
- ↑ Smith 2022a, p. 137–143.
- ↑ Adamson 2007, p. 479–48.
- ↑ Smith 2008, p. 176–178.
- ↑ Hartz 2009, p. 106–108.
- ↑ Smith 2008.
- ↑ Momen 2019b.
- ↑ Universal House of Justice 2013.
- ↑ Hartz 2009, p. 56–63.
- ↑ Smith 2008, p. 21–22.
- ↑ Warburg 2006, p. 144–145, 178.
- ↑ Bolodo-Taefi 2022a, p. 258–267.
- ↑ Hartz 2009, p. 86.
- ↑ Sergeev 2022, p. 270–272, 274–276, 277–279.
- ↑ Warburg 2006, p. 13.
- ↑ Saiedi 2000, p. 98.
- ↑ Smith 2000, p. 79–80.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 40.
- ↑ Smith 2008, p. 25–26.
- ↑ Effendi 1944, p. 158–159.
- ↑ Smith 2008, p. 28–29.
- ↑ Adamson 2007, p. 384–385.
- ↑ Smith 2008, p. 28–31.
- ↑ Hatcher & Martin 1984, p. 45–46.
- ↑ Smith 2000, p. 100–101, 307.
- ↑ Universal House of Justice 1993.
- ↑ Hartz 2009, p. 56.
Marejeleo
Maudhui ya Kibaha'i
- Jumuiya ya Kimataifa ya Baha'i (2019). "Picha ya Bahá'u'lláh". Maisha ya Baháʼu'lláh – Simulizi la Picha. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
- Taherzadeh, Adib (1980). Picha za Baháʼu'lláh; William Miller. Oxford, UK: George Ronald. ISBN 0-85398-439-5. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
{{cite book}}: More than one of|author=na|last=specified (help); More than one of|location=na|place=specified (help) - Nyumba ya Haki ya Ulimwengu (1993). "Maktaba za Baháʼí: Kuhifadhi na Kulinda Maandishi Matakatifu". Andalib. 12. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
- Nyumba ya Haki ya Ulimwengu (1999). "Picha ya Baha'u'llah kwenye Tovuti". Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
- Nyumba ya Haki ya Ulimwengu (2013). "Nambari na Aina za Maandishi na Maandishi Matakatifu". Lights of Irfan. 10. Wilmette, IL: Irfan Colloquia. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
Kamusi elezo
- Bausani, A. (2011). "AQDAS". Encyclopædia Iranica. Juz. la II, Fasc. 2. ku. 191–192.
- Bausani, A.; MacEoin, D. (2011). "ʿAbd-Al-Bahāʾ". Encyclopædia Iranica. Juz. la I, Fasc. 1. ku. 102–104.
- "Bahāʾī Faith". Encyclopædia Britannica. 13 Desemba 2022. Iliwekwa mnamo 2022-01-01.
- Hornby, Helen, mhr. (1988). Lights of Guidance: A Baháʼí Reference File (tol. la Toleo la pili lililorekebishwa na kuongezwa). New Delhi: Baháʼí Publishing Trust. ISBN 81-85091-46-3.
- Smith, Peter (2000). A Concise Encyclopedia of the Baháʼí Faith. Oxford, Uingereza: Oneworld Publications. ISBN 1-85168-184-1.
- Kigezo:Encyclopedia
Vyanzo Vingine
- Adamson, Hugh (2007). Historical Dictionary of the Baháʼí Faith. Oxford, UK: Scarecrow Press. ISBN 978-0-8108-3353-1.
- Alkan, Necati (2022). "Ch. 6: 'Abdu'l-Bahá 'Abbás". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 72–87. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Amanat, Mehrdad (2011). Jewish Identities in Iran: Resistance and Conversion to Islam and the Baha'i Faith. I.B. Tauris. ISBN 978-1845118914.
- Balyuzi, Hassan (28 Septemba 2009). Religions – Baháʼí: Baháʼu'lláh. Oxford, UK: BBC News. ISBN 0-85398-328-3. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
{{cite book}}: More than one of|author=na|last=specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - BBC (28 Septemba 2009b). "Religions – Baháʼí: The Báb". BBC News. Iliwekwa mnamo 2022-12-23.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - de Bellaigue, Christopher (2018). The Islamic Enlightenment: The Modern Struggle Between Faith and Reason. London: Vintage. ISBN 978-0-099-57870-3.
- Bolodo-Taefi, Vargha (2022). "Ch. 14: God, Revelation, and Manifestation". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 175–187. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Bolodo-Taefi, Vargha (2022a). "Ch. 22: Mysticism". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 258–268. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Buck, Christopher (2004). "The eschatology of Globalization: The multiple-messiahship of Bahā'u'llāh revisited". Katika Sharon, Moshe (mhr.). Studies in Modern Religions, Religious Movements and the Bābī-Bahā'ī Faiths. Boston: Brill. ku. 143–178. ISBN 90-04-13904-4.
- Buck, Christopher (24 Oktoba 2019). "Bahá'í Social Principles First Proclaimed by the Báb". BahaiTeachings.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - Cole, Juan (1982). "The Concept of Manifestation in the Baháʼí Writings". Baháʼí Studies. monograph 9: 1–38.
- Dehghani, Sasha (2022). "Ch. 15: Progressive Revelation". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 188–200. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Elwell-Sutton, L.P. (1976). "Review of "The Baha'i Faith" Its History and Teaching by William McElwee Miller". Journal of the Royal Asiatic Society of Great Britain and Ireland. 108 (2): 157–158. doi:10.1017/S0035869X00133416. JSTOR 25203713. S2CID 162531277.
- Hartz, Paula (2009). World Religions: Baha'i Faith (tol. la 3rd). New York: Chelsea House Publishers. ISBN 978-1-60413-104-8.
- Hatcher, John (1997). The Ocean Of His Words: A Reader's Guide to the Art of Bahá'u'lláh. Wilmette, IL: Baháʼí Publishing Trust. ISBN 0-87743-259-7.
- Hatcher, William; Martin, Douglas (1984). The Baháʼí Faith: The Emerging Global Religion. San Francisco, CA: Harper and Row. ISBN 0-06-065441-4.
- Heller, Wendy M. (2022). "Ch. 34: The Covenant and Covenant-Breaking". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 409–425. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Hollinger, Richard (2022). "Ch. 8: Shoghi Effendi Rabbani". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 105–116. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Ma'ani, Baharieh Rouhani (2008). Leaves of the Twin Divine Trees. Oxford, UK: George Ronald. ISBN 978-0-85398-533-4.
- Kluge, Ian (2022). "Ch. 19: The Physical and Spiritual Dimensions of Human Nature". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 230–239. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Mahmoudi, Hoda (2022). "Ch. 32: Peace". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 384–393. doi:10.1163/ej.9789004170353.i-740. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Maneck, Susan (1990). "Conversion of Religious Minorities to the Baha'i Faith in Iran: Some Preliminary Observations". Journal of Bahá'í Studies. 3 (3). Iliwekwa mnamo 2012-03-28.
- Maneck, Susan (1984). "Early Zoroastrian Conversions to the Bahá'í Faith in Yazd, Iran". Katika Cole, Juan Ricardo; Momen, Moojan (whr.). Studies in Bábí and Bahá'í history. Juz. la 2 of Studies in Babi and Baha'i History: From Iran East and West (tol. la illustrated). Kalimat Press. ku. 67–93. ISBN 978-0933770409.
- Matthews, Gary (2005). The Challenge of Baháʼu'lláh: Does God Still Speak to Humanity Today?. Wilmette, IL: Baháʼí Publishing. ISBN 1-931847-16-9.
- Momen, Moojan, mhr. (1981). The Bábí and Baháʼí Religions, 1844–1944: Some Contemporary Western Accounts. Oxford, UK: George Ronald. ISBN 0-85398-102-7.
- Momen, Moojan (23 Septemba 2019a). "Baha'i Faith and Holy People". Katika Jestice, Phyllis G. (mhr.). Central Figures of the Bahaʼi Faith. Santa Barbara, CA: ABC-CLIO. ISBN 1-57607-355-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Oktoba 2020.
{{cite book}}:|website=ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Momen, Moojan (23 Septemba 2019b). "Bahaʼi Sacred Texts". British Library: Discovering Sacred Texts. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Desemba 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - Mount, Guy Emerson (2022). "Ch. 20: Unity in Diversity". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 240–246. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Nakhjavani, Bahiyyih (1983). Four on an Island. Oxford, UK: George Ronald. ISBN 0-85398-174-4.
- Pearson, Anne M. (2022). "Ch. 21: The Equality of the Sexes". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 247–257. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Phelps, Steven (2022). "Ch. 5: The Writings of Baháʼuʼlláh". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 51–71. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Saiedi, Nader (2008). Gate of the Heart: Understanding the Writings of the Báb. Waterloo, ON: Wilfrid Laurier University Press. ISBN 978-1-55458-035-4.
- Saiedi, Nader (2000). Logos and Civilization: Spirit, History and Order in the Writings of Bahá'u'lláh. Bethesda, MD: University Press of Maryland. ISBN 1-88305-363-3.
- Salmání, Ustád Muhammad-ʻAlíy-i (1982). My Memories of Baháʼu'lláh. Los Angeles, CA: Kalimát Press.
- Schaefer, U.; Towfigh, N.; Gollmer, U. (2000). Making the Crooked Straight: A Contribution to Baháʼí Apologetics. Oxford, UK: George Ronald. ISBN 0-85398-443-3.
- Sergeev, Mikhail (2022). "Ch. 23: Progress of the Soul: Life After Death". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 269–281. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Sharon, Moshe (2011-01-13). "Jewish Conversion to the Baha?i faith". Chair in Baha'i Studies Publications. The Hebrew University of Jerusalem. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-20. Iliwekwa mnamo 2012-03-28.
- Smith, Todd (2022a). "Ch. 11: The Universal House of Justice". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 134–144. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Smith, Todd; Ghaemmaghami, Omid (2022b). "Ch. 37: Consultation". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 450–462. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Sours, Michael (1991). Understanding Christian Beliefs. Oxford, UK: Oneworld Publications. ISBN 1-85168-032-2.
- Stockman, Robert (8 Julai 2008). "Ch. 18: Oneness and Unity". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). Baháʼí Holy Places in Haifa and the Western Galilee. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 219–229. ISBN 978-1-138-36772-2. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2021.
{{cite book}}: More than one of|author=na|last=specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - White, Christopher (2022). "Ch. 24: Bahá'í Spirituality and Spiritual Practices". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). The World of the Bahá'í Faith. Oxfordshire, UK: Routledge. ku. 282–288. ISBN 978-1-138-36772-2. OCLC 234309958.