Asela wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Asela wa Roma (Roma, Italia, 334 hivi - Roma, 406 hivi) alikuwa bikira Mkristo wa mji huo aliyeishi tangu umri wa miaka 10 hadi uzeeni katika kufunga na kusali, kama alivyohimizwa na Atanasi wa Aleksandria[1].

Jeromu alimsifu sana na kumuita "Ua la Bwana"[2].

Juu yake aliandika pia Paladi, askofu mwanahistoria aliyemtembelea katika chumba chake kidogo mjini. Toka huko alikuwa akiongoza monasteri[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 6 Desemba[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Dunbar, Agnes B.C. (1901). A Dictionary of Saintly Women. Volume 1. London: George Bell & Sons, pp. 85-86
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.