Nenda kwa yaliyomo

Apoloni wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Apoloni wa Roma (Roma, Italia, karne ya 2 - Roma, 21 Aprili 185) alikuwa mwanafalsafa wa ukoo maarufu ambaye alitetea Ukristo hata kwa maandishi na kwa sababu hiyo aliuawa katika dhuluma ya kaisari Commodus.

Baada ya kuutetea mbele ya gavana Pereni na ya Senati ya Dola la Roma kwa hotuba fasaha, aliuthibitisha ukweli wake kwa ushahidi wa damu yake[1].

Habari zake tumezipata kutoka kwa mwanahistoria Eusebi wa Kaisarea, Jeromu na wengineo[2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Aprili[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90522
  2. Enciclopedia dei Santi: Sant'Apollonio di Roma
  3. "saintpatrickdc.org". www.saintpatrickdc.org.
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.