Anne Curtis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
{{{jina}}}
Jina la kuzaliwa Anne Marie Ojales Curtis Smith
Alizaliwa 17 Februari 1985
Australia
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Anne Curtis

Anne Curtis (jina halisi Anne Marie Ojales Curtis Smith alizaliwa nchini Australia 17 Februari 1985) ni mwanamitindo wa Kifilipino-Kiaustralia na msanii maarufu nchini Ufilipino.

Amejipatia umaarufu zaidi baada ya kucheza kama Celine Magsaysay katika tamthilia ya Maging Sino Ka Man na kama Imang au Fatima, mhusika mkuu katika Kampanerang Kuba.

Tamthilia zote hizi zilirushwa hewani na mtandao wa ABS-CBN iliyopo nchini Ufilipino. Anne alikuja kuwa mshindi wa kwanza kwenye tuzo za MYX 2005 baada ya kufanya vizuri kwenye video ya muziki aliyoshirikishwa ya I need You ya Mark Bautista.

Mnamo 2007 Anne alikuja kuwa MTV VJ kwenye MTV ya Ufilipino iliyoanzishwa tarehe 1 Machi 2007. Kwa sasa anaigiza kwenye filamu mpya akiwa na Aga Muhlach chini ya Star Cinema na tamthilia mpya na Zanjoe Marudo kama mwenza.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Curtis alizaliwa na kulelewa Australia na mama wa Kifilipino na baba wa Kiaustralia.

Aliishi Australia hadi baba yake (ambaye ni mwanasheria), James Curtis, alipohamia Ufilipino wakati Anne alikuwa ana umri wa miaka 12. Kuhamia Ufilipino ni hatua ambayo Curtis anaishukuru sana. “Nina furaha sana kuwa hapa. Kama ingekuwa ni Australia ningekuwa shule ya bweni! Baba yangu ni ‘mkali’ sana kwenye mambo ya Elimu. Alikuwa ananikemea pale nilipojihusisha na mambo ya biashara, akidai kuwa yalikuwa yananivutia kutoka shuleni. Tuliishi tukilala saa 2 au 3 usiku. Kusema kweli sikuyafurahia maisha yale. Lakini hapa kuna vivutio vingi vya kufurahisha. Kama kijana nimeamua kuishi hapa (Ufilipino) lakini pindi nitakapotulia na kutafakari, nitarudi Australia. "[1] Hivi sasa, yeye ana blog mafanikio katika LOOKBOOK.NU.

Uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Uigizaji wa awali[hariri | hariri chanzo]

Alijizolea mashabiki hasa katika maigizo yake yanayohusisha zaidi mapenzi, pale alipounganishwa na Richard Gutierrez.

Uhusika uliochangia mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2004, alipohamia ABS-CBN, Curtis alianza kwa kishindo kuiingia sanaa ya tamthilia pale alipoigiza kama Stephanie Borromeo kwenye tamthilia ya ‘’Hiram’’ kama rafiki kipenzi na adui wa mapenzi wa Magret Benipayo nafasi iliyoigizwa na Heart Evangelista.

Mnamo mwaka 2005, mafanikio ya kuigiza vema kwenye ‘’Hiram’’ yalipelekea kupewa nafasi ya uhusika mkuu kama Imang/Fatima kwenye tamthilia ya ‘’Kampanerang Kuba’’.[2].

Mnamo mwaka 2006, Curtis alirudi tena kwenye anga ya tamthilia kama ‘’Celine Magsaysay’’ katika ‘’Maging Sino Ka Man’’, safari hii aliunganishwa na ‘’ Sam Milby’’ kutoka ‘’Pinoy Big Brother’’.

Kashfa[hariri | hariri chanzo]

‘’’Video ya kwenye simu za kiganjani na aliyekuwa mpenzi wake ‘’Richard Gutierrez’’

Curtis na uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake na msanii ‘’Richard Gutierrez’’ ulikuja kuwa kiini cha uvumi hasa baada ya video kutoka kwenye simu yake ya mkononi (ikionyesha wawili hao wakiwa kwenye mkao wa kimahaba) kuanza kusambaa kupitia barua pepe na ujumbe wa simu za mkononi(MMS).[3] Simu yake ilipotea na kusababisha hiyo video kusambaa kwenye umma.

Curtis bila hiyana alikiri kuhusiana na video hiyo ya simu: “Sioni sababu ya kukataa,” alifafanua. “Mimi sio mtu mwenye tabia ya ‘kuruka’ kitu chochote. Nitaonekana kama muongo.” [1]

Kujiandikia jina kibiashara kwa unywaji wa vileo

Kwenye mkutano mnamo Aprili 2005, Curtis alielezea uamuzi wake uliopelekea kuzua mabishano wa kusahihisha kibiashara GSM Blue, kinywaji chenye kilevi: "Nimeshasema mara nyingi kabla, sababu ya mimi kufanya biashara ile ilikuwa nitokapo mwenyewe sikatai kuwa mimi ni nakunywa, lakini unywaji wa kawaida na sio ulevi. Juu ya hayo, Nahitaji fedha kwa ajili ya mahitaji yangu ya kila siku, papano ako mabubuhay? Sijali kama inajenga mfano mbaya kwa vijana wadogo. Kwa watu wengine, ijapokuwa, hawaoni kuwa tayari nina miaka 20,"[1]

Maigizo[hariri | hariri chanzo]

Tamthiliya[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Kama
2008 The Wedding (TV series)
2008 Love Spell Presents: The Face Shop Pearl
2007 Maging Sino Ka Man: Book 2 Celine Magsaysay
2007 Your Song: Ikaw Allison
2007 Sineserye Presents: May Minamahal Monica Fernandez
2007 Your Song: Someone In The Dark Lalaine
2007 MTV Gimme Ten VJ
2007 MTV Timeout VJ
2006 Maging Sino Ka Man Celine Magsaysay
2006 Star Circle Summer Kid Quest Host
2006 Love Spell Presents: Wanted Mr. Perfect Rowena
2006 Maalaala Mo Kaya: Bisikleta
2006 Komiks: Alpha Omega Girl Alpha Omega Girl
2006 Maalaala Mo Kaya: Salamin Moni
2006 Komiks: Mamayang Hatinggabi Beba
2006 Your Song: I'll Never Get Over You (Getting Over Me) Ana
2005 Pinoy Big Brother Buzz Host
2005 The Buzz Segment Host
2005 Kampanerang Kuba Imang/Fatima/Bernadette
2005 Qpids Host
2004 Hiram Stephanie Borromeo
2004 ASAP Host/Performer
2003 Nuts Entertainment Herself
2003 Love To Love: My 1, 2 Love! Casey de Leon
2002 SOP Performer
2002 Ang Iibigin Ay Ikaw Rosana
2001 Kakabakaba: Chaka Doll Monica
2001 Beh! Bote Nga!
2000 Hati-hating Kapatid
1999 May Bukas Pa Karen
1997 Mornings at GMA Host
1997 Ikaw na Sana Jasmin
1996 Anna Karenina Ginny
1995 TGIS Emily/Em

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Kama
2008 Waiting For Your Love TBA with (Aga Mulach)
2007 Ang Cute ng Ina Mo Christine
2006 Wag Kang Lilingon Melissa
2006 All About Love Badong
2003 Filipinas Lyra
2003 Alab Ng Lahi
2003 Lastikman Young Linda
2002 Akala Mo
2002 Mahal kita: Final Answer! Leslie
2000 Juan & Ted: Wanted Ibong Adarna
2000 Ika-13 Kapitulo Angela
1999 Honey, My Love, So Sweet
1997 Magic Kingdom

Mahusiano[hariri | hariri chanzo]

Oyo Boy Sotto[hariri | hariri chanzo]

Baada ya miezi sita ya uchumba, Curtis aliingia kwenye uhusiano wa miaka miwili na aliyekuwa mpenzi wake Oyo Boy Sotto, mtoto wa mwanamitindo maarufu Vic Sotto na Dina Bonnevie. Oyo 'Boy' Sotto ni muigizaji. Curtis ananuelezea uhusiano wake na Sotto kama mara yake ya kwanza kuwa kwenye mapenzi sahihi, akimuongelea Sotto: "Yeye ndiye ambaye nilimpenda kwa dhati."[4] Ilipofika Juni 2003, uhusiano wao ulivunjika rasmi. Katika mahojiano baadaye, Sotto alilaumu "Utoto na wazimu" kama chachu ya wao kushindwa kulilea penzi lao.

Richard Gutierez[hariri | hariri chanzo]

Curtis pia alikuwa na uhusiano wa wazi na muigizaji mwenzie Richard Gutierez mnamo mwaka 2004. Wawili hao walishiriki pamoja kwenye vipindi vya maonyesho ya Nuts Entertainment na Love to Love.

Paolo Araneta[hariri | hariri chanzo]

Curtis baadaye alikuja kuhusishwa na mahusiano ya kimapenzi na Paolo Araneta, uhusiano uliodumu kwa miaka miwili. Mnamo Januari 2006, walakini, vyanzo vya habari upande wa burudani vilithibitisha kuwa Curtis na Araneta walikuwa wameachana.[5]. Hakuna sababu rasmi iliyotolewa.

Pia kuna baadhi ya vyanzo vinamhusisha na Sam Milby. Muigizaji mwenza kwenye masula ya mapenzi wa Anne Curtis kwenye tamthilia ya Maging Sino Ka Man. Ambayo imemalizika hivi karibuni. Ila kuna muendelezo wake(kitabu cha pili) unakuja hivi karibuni kwenye mwaka huu. Curtis alinukuliwa akisema kuwa wao ni marafiki tu lakini hakuna anayejua baadaye nini kitatokea. Curtis pia alisema kuwa anavutiwa na Sam.

Moyo wa huruma[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2005, Curtis alishiriki kwenye azimio la kutolea kusaidia kwa kuwatembelea watoto huko Pampanga ambao wamefanyiwa upasuaji wa kaakaa la kinywa lenye mpasuko. Ujuzi alioupata ulimsukuma na akasikika akisema "sasa nataka kusaidia zaidi."[6]

Matangazo ya biashara na taswira[hariri | hariri chanzo]

  • Smart Telecommunications
  • GSM Blue - 2005[6]
  • Rexona Sensive
  • Watch Republic
  • Colgate
  • Head & Shoulders
  • Monde
  • Freego
  • Belo Medical Group
  • Freeway

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]