Anastazia wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malkia Theodora na wapambe wake.

Anastazia wa Aleksandria (kwa Kilatini: Anastasia Patricia; alifariki 576) alikuwa mwanamke wa ikulu huko Bizanti na hatimaye mmonaki huko Misri.[1]

Alikuwa mpambe wa malkia Theodora wa Bizanti[2], mke wa kaisari Justinian I. Theodora alipoanza kumuonea wivu[1], Anastazia aliamua kuhamia Aleksandria.[1] Huko Pempton alianzisha monasteri alipofuata nidhamu na kujitegemea kwa kufuma nguo.[1]

Theodora alipofariki mwaka 548, Justinian alitaka Anastazia arudi Konstantinopoli, lakini bure.[1] Badala yake, Anastazia alikwenda Skete asaidiwe na Danieli, abati wa huko.[3][1] Hapo Anastasia alifichama katika laura (chumba cha kimonaki) umbali wa kilometa 29 akivaa kanzu ya kiume[1] na kuishi kama mkaapweke wakati hilo lilikubalika kwa wanaume tu. Danieli alimtembelea kila wiki na kuhakikisha mwanafunzi wake mwingine anampatia maji.[1] Anastasia dwelt in seclusion for twenty-eight years.[1]

Mwaka 576[4] Anastazia alimuarifu Danieli kwamba amekaribia kifo[1] naye akamletea Ekaristi na kupokea maneno yake ya buriani.[3][1] Ndipo alipomueleza ukweli mwanafunzi yule[5] .

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Machi[1] ila kwa Wakhufi ni tarehe 26 Tobi[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 Laura Swan, The Forgotten Desert Mothers (2001, ISBN 0809140160), pages 72-73
  2. Anne Commire, Deborah Klezmer. Women in World History: A Biographical Encyclopedia (1999, ISBN 0787640808), page 274.
  3. 3.0 3.1 "St. Anastasia the Patrician of Alexandria", Antiochian Orthodox Christian Archdiocese
  4. Coquin, Rene Georges. "Anastasia, Saint", The Coptic Encyclopedia, Vol. I, MacMillan (1991)
  5. Her story survives in one recension of the Copto-Arabic Synaxarion and by a tale of Daniel of Scetis.
  6. http://www.copticchurch.net/synaxarium/5_26.html#2

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.