Amman
Amman nchini Yordani | |
Mkoa | Mkoa wa Amman |
Anwani ya kijiografia | Latitudo: 31º57'00" N - Longitudo: 035º 55' 59" E |
Kimo | 773 m juu ya UB |
Eneo | ?? km² |
Wakazi | milioni 4 |
Msongamano wa watu | watu 2,380 kwa km² |
Simu | +962 (nchi), 6 (mji) |
Mahali | |
Amman (kwa Kiarabu: عمان ʿammān) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Yordani wenye wakazi milioni nne katika rundiko la mji.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Mji uko takriban km 40 kutoka ncha ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi kati ya vilima vya Yordani ya kaskazini-magharibi.
Hali ya hewa ni afadhali kushinda mahali pengi pa Yordani kwa sababu ya kimo cha mji, hivyo joto halizidi mno.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Amman ni mji wenye historia ndefu iliyojulikana kwa jina la Rabat Amon wakati wa Biblia.
Ilistawi vizuri hadi nyakati za Dola la Roma ilipopambwa na majengo makubwa na mazuri yanayoonekana hadi leo.
Lakini umuhimu wake ulipungua siku za Wamuawiya na wakati wa kuundwa kwa Yordani palikuwa kijiji tu. Mfalme Abdullah bin al-Husayn alianzisha hapa mji mkuu wake. Hadi vita kuu ya pili ya dunia Amman haikuzidi wakazi 30,000.
Lakini mji ulikua haraka baada ya kuundwa kwa Israel kwa sababu wakimbizi wengi kutoka sehemu za Palestina zilizokuwa Israel walikimbilia Amman.
Kipindi cha pili cha kukua kilitokea tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanoni miaka ya 1975-1990. Sehemu kubwa ya benki na biashara kutoka Beirut ilihamia Amman iliyoendelea kuwa kitovu kipya cha biashara na uchumi upande wa mashariki wa Mediteranea.
Picha za Amman
[hariri | hariri chanzo]-
Amman mjini mwaka 2002
-
Msikiti wa Abu Darweesh
-
Uwanja wa maigizo ya Kiroma
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Amman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |