Alpha Centauri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Alpha Centauri katika kundinyota ya Kentaurus

Alpha Centauri (pia: Toliman au Rigil Kentaurus) ni nyota inayong'aa sana katika anga ya kusini kwenye kundinyota ya Centaurus. Ni nyota ya kungaa sana ya nne angani lakini haionekani kwenye nusudunia ya kaskazini.

Alpha Centauri ni nyota ya pekee kwa sababu ni nyota yetu jirani katika anga ina umbali wa miaka ya nuru 4.2 - 4.2.

Mfumo wa nyota[hariri | hariri chanzo]

Uhusiano wa ukubwa wa nyota za Kentaurus na jua letu

Alpha Centauri ni sehemu ya mfumo wa nyota tatu. Nyota mapacha za Alpha Centauri A na Alpha Centauri B ziko miaka ya nuru 4.36 kutoka kwetu na nyota ya tatu Proxima Centauri ina umbali wa miaka ya nuru 4.22.