Mshubiri
Kwa kipimo chenye jina la karibu angalia hapa shubiri
Mshubiri (Aloe spp.) | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mlalangao (Aloe lateritia)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi ±450: |
Mshubiri au msubili ni jina la mimea ya jenasi Aloe katika nusufamilia Asphodeloideae ya familia Xanthorrhoeaceae ambayo ni aina za sukulenti. Watu wengi wanaendelea kuweka Aloe ndani ya familia yake Aloaceae. Spishi kadhaa ni miti, lakini siku hizi huainishwa katika jenasi Aloidendron.
Majani ya mishubiri na dawa zilizotengenezwa kutoka haya huitwa shubiri.
Mimea hii ina shina fupi au haina shina kabisa, isipokuwa spishi zilizo miti. Majani ni marefu na manono na yanatoka shina karibu na wenziwe; yana miiba kingoni mwao. Maua yana umbo wa mrija mfupi na rangi yake ni nyekundu, pinki, ya machungwa, njano au nyeupe. Yapo mwishoni mwa kikonyo chenye vitawi au bila vitawi. Utomvu utokao mwenye majani hutumika kutengeneza dawa.
Spishi moja inajulikana sana: mshubirimani (Aloe vera), ambao unapandwa sana duniani na hutumika kwa kutengeneza dawa za uganga au za mitishamba.
Spishi nyingine inayopandwa sana katika Afrika na nchi nyingine za Tropiki ni mshubiri mwekundu (A. ferox).
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Aloe ballyi, Mshubiri wa Bally
- Aloe carolineae, Mshubiri wa Carol
- Aloe chabaudii, Mshubiri wa Chabaud
- Aloe christianii, Mshubiri wa Christian
- Aloe citrina, Mshubiri Njano
- Aloe dawei, Mshubiri wa Dawe
- Aloe duckeri, Mshubiri wa Ducker
- Aloe elgonica, Mshubiri wa Elgoni
- Aloe ferox, Mshubiri Mwekundu
- Aloe flexilifolia
- Aloe kedongensis, Kiruma
- Aloe kilifiensis, Mshubiri wa Kilifi
- Aloe lateritia, Mlalangao
- Aloe microdonta
- Aloe ngongensis, Mshubiri wa Ngong
- Aloe nuttii, Kisimamleo
- Aloe nyeriensis, Mshubiri wa Nyeri
- Aloe rabaiensis, Jolonji
- Aloe rivae
- Aloe ruspoliana, Mshubiri wa Ruspol
- Aloe scabrifolia
- Aloe secundiflora, Mshubiri-nyani
- Aloe turkanensis, Mshubiri Turkana
- Aloe tweediae
- Aloe ukambensis, Mshubiri Kamba
- Aloe vera, Mshubirimani
- Aloe volkensii
- Aloe wilsonii, Mshubiri wa Wilson
- Aloe wollastonii, Mlalangao
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mshubiri wa Chabaud
-
Mshubiri wa Christian
-
Mshubiri wa Dawe
-
Mshubiri wa Elgoni
-
Mshubiri mwekundu
-
Kiruma
-
Mshubiri wa Nyeri
-
Jolonji
-
Aloe rivae
-
Mshubiri-nyani
-
Mshubiri Kamba
-
Shibirimani
-
Aloe volkensii
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mshubiri kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |