Alisson Becker

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Alisson akiwa golini na timu yake ya taifa

Alisson Ramses Becker (anayejulikana sana kama Alisson; alizaliwa 2 Oktoba 1992) ni mchezaji wa soka wa Brazili ambaye anacheza kama golikipa wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool FC na timu ya taifa ya Brazili.

Alisson alianza kazi yake na Internacional, ambapo alicheza mechi zaidi ya 100 na alishinda Campeonato Gaúcho katika kila msimu. Mnamo mwaka 2016, alihamia AS Roma kwa dau la milioni 7.5.

Mnamo Julai 2018, Alisson alijiunga na Liverpool kwa ada ya milioni 62.5, ambayo iliweza kuongezeka kuwa euro milioni 72.

Alisson aliiwakilisha Brazili katika viwango mbalimbali vya vijana kabla ya kuanza mwanzo wake wa kimataifa mwaka 2015 ambapo baadae aliliwakilisha taifa lake katika Copa América Centenario mwaka 2016 na Kombe la Dunia la FIFA 2018.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alisson Becker kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.