Nenda kwa yaliyomo

Mtunguru (mmea)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aframomum)
Mtunguru
Mtunguru wa Zambesi (Aframomum zambesiacum)
Mtunguru wa Zambesi (Aframomum zambesiacum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Zingiberales (Mimea kama mtangawizi)
Familia: Zingiberaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mtangawizi)
Jenasi: Aframomum
K.Schum.
Ngazi za chini

Spishi 50

Mitunguru, mitungulu, mitunguu au miiliki mwitu ni mimea ya kudumu ya jenasi Aframomum katika familia Zingiberaceae (familia ya mtangawizi). Mbegu za spishi nyingi hutumika kama kiungo ambacho ladha yake inafanana na pilipili manga au iliki.

Mimea hiyo hutokea Afrika kusini mwa Sahara. Ina mashinaukoka ambayo hutoa mashina marefu ya hadi m 2 au zaidi kutoka kwa mafundo yao. Mashina hayo yanabeba majani yasiyoelekeana hadi sm 30 kwa urefu. Maua hukua kwa vishada kwenye mashina mafupi yanayotoka moja kwa moja kutoka kwa shinaukoka.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]