Fundo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fundo kati ya kamba ya buluu na nyekundu.
Mafundo ya mabaharia.

Fundo (Kiing. knot) ni namna ya kuunganisha pande mbili za kamba, uzi au kitambaa, dutu kinamo kama mpira au wakati mwingine pia za nyororo.

Namna ya kupinda pande mbili kati yake inaongeza uso zinapogusana na hivyo kuongeza msuguano wakati pande mbili zinavutwa; msuguano huo unazuia kuteleza kwa kamba juu ya kamba. Kila fundo linapokazwa huwa imara zaidi.

Mafundo yamepatikana tangu kale, wakati binadamu walianza kutumia vikonyo vya mimea au nyuzi nyingine kufunga mawe kwenye pini za shoka zao. Mafundo yalitumiwa pia kwa kutengeneza nyavu au matego.

Mafundo yaliendelea sana kuwa tata tangu kupatikana kwa mashua ya tanga.

Kati ya mabaharia elimu ya mafundo imekuwa sayansi ya pekee. Walijifunza na kufundishana kutumia mafundo mbalimbali kwa shughuli maalumu.

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: