Adriani wa Canterbury

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Adriani wa Canterbury, O.S.B. (alifariki 9 Januari 710) alikuwa mmonaki msomi na hatimaye kwa miaka 39 abati huko Canterbury, Kent, Uingereza.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Beda Mheshimiwa, alikuwa Mberberi[2] kutoka Afrika Kaskazini.

Baada ya kuongoza monasteri karibu na Napoli, Papa Vitalian alimteua mara mbili kuwa askofu mkuu wa Canterbury, lakini alikataa akipendekeza wengine.

Theodoro wa Tarso alipokubali, Vitalian alimuagiza Adriani aongozane naye kwenda Britania, kwa sababu alijua njia hadi Galia.

Theodoro alifika huko 669, kumbe Adriani alizuiwa kwa muda, lakini alipofika tu Canterbury alifanywa abati kama Papa alivyokuwa ameagiza.

Adriani akiwa maarufu kwa ujuzi wake wa Biblia, Kigiriki na Kilatini [3], pamoja na kuwa kiongozi bora, alifanya monasteri yake kuwa na athira kubwa.[4]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
  2. Serralda, Vincent (1984-01-01). Le Berbère-- lumière de l'Occident (in fr). Nouvelles Editions Latines, 147. ISBN 9782723302395. 
  3. Lapidge, Michael (2006). The Anglo-Saxon Library. Oxford: Oxford UP, 33, 87–88. ISBN 9780199239696. 
  4. Bede, Historia ecclesiastica gentis Anglorum iv. 1, 2.; and Vita Abbatum Wiramuth., in Smith's Beda, p. 293.; W. Malmes. De Pontif. p. 340.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Long, George. The Biographical Dictionary of the Society for the Diffusion of Useful Knowledge. London: Longman, Brown, Green & Longmans, 1842-1844. 4 vols.
  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adriani wa Canterbury kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.