Nenda kwa yaliyomo

Aderaldo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aderaldo (Troyes, Ufaransa, karne ya 10 - 20 Oktoba 1004) alikuwa padri kanoni na shemasi mkuu wa jimbo lake la asili.

Aliinua hali ya monasteri kadhaa kwa mafundisho yake na uaminifu wake alioushika hata alipotekwa na maharamia Waislamu wakati alipohiji Nchi takatifu.

Aliporudi alianzisha monasteri ya kwake [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki[2] na Waorthodoksi[3] kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Oktoba[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Estienne Binet, De la sainte hiérarchie de l’Église, et la vie de saint Adérald, S. Cramoisy, 1633
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.