Sanaa isiyoshikika
Sanaa isiyoshikika ni sanaa ya kisasa ambayo hailengi kuonyesha picha za dunia yetu ya kila siku. Inatumia rangi, mistari na maumbo (fomu), lakini si kwa nia ya kuwakilisha vitu au viumbe vilivyo hai. Mara nyingi wasanii wa aina hiyo waliathiriwa na maoni na falsafa za kutoshikika.
Sanaa isiyoshikika hupatikana hasa katika uchoraji na uchongaji. Pia kuna kazi nyingi za sanaa ambazo kwa sehemu hazishikiki, na kwa sehemu zinawakilisha uhalisia. Wasanii wengi walifanya kazi kwa aina ya sanaa ya kisasa na aina nyingine.
Sanaa isiyoshikika ni uvumbuzi wa karne ya 20. Ilikuwa kati ya aina za kwanza za sanaa ya kisasa, lakini labda ni harakati moja ambayo ni ya kisasa kabisa. Haina mizizi katika sanaa ya mapema (kama tunavyotumia neno leo). [1]
Mianzo
[hariri | hariri chanzo]Mmoja wa kwanza aliyechora picha isiyoshikika kabisa alikuwa Kazimir Malevich, ambaye aliwasilisha mraba mweusi kabisa mnamo 1913. Katika sanaa yake aliyoitumia tu tangu na maumbo ya kijiometri.
Kuna mamia ya wasanii ambao walichora kazi zisizoshikika. Piet Mondrian na mchongaji Henry Moore wanastahili kutajwa kwa ushawishi wao mkubwa kwa wasanii wengine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Just possibly some prehistoric art might be counted. Islamic decorative tiles in early mosques might be a candidate.