Nenda kwa yaliyomo

Paradiso : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'right|thumb|[[Nicolas Poussin, ''Majira manne ya paradiso'', 16601664.]] Image:Jan Bruegel d. Ä. 003.jpg|thumb|2...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:45, 22 Desemba 2015

Nicolas Poussin, Majira manne ya paradiso, 16601664.
Paradiso kadiri ya Jan Bruegel.

Paradiso (kutoka Kiajemi: پردیس, bustani) ni jina la mahali pa amani kamili.

Dini za Abrahamu zinatumia jina hilo kwa Eden, yaani ulimwengu wa kabla ya dhambi ya asili, na vilevile kwa ule unaotarajiwa kuwepo milele.

Asili ya jina

Neno "paradiso" limeenea katika lugha nyingi (paradis, paradisus, paradise n.k.) kupitia Kigiriki parádeisos (παράδεισος), kutoka Kiajemi cha zamani *paridayda- "eneo lililozungukwa na uzio".

Katika Agano la Kale

Katika Kiebrania פרדס (pardes) inapatikana mara tatu katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania): Wimbo Ulio Bora 4:13, Mhubiri 2:5 na Nehemia 2:8.

Katika Agano Jipya

Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo neno linapatikana vilevile mara tatu: Luka 23:43 (Yesu msalabani alilitumia akimjibu mhalifu aliyetubu ili kumhakikishia watakuwa pamoja), 2 Kor 12:4 (Mtume Paulo alilitumia kuelezea hali ya pekee aliyojaliwa kwa njozi, Ufunuo 2:7 (kuhusiana na Mwa 2:8 na mtu wa uzima.

Katika Uislamu

Kwa Kiarabu na katika Quran inaitwa فردوس., firdaus.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.