Waborana
Mtu mwenye asili ya Kiborana akipiga kura katika kituo cha upigaji kura Marsabit, Kenya. |
| Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana |
|---|
| Ethiopia, Kenya |
- Borana pia ni jina la Kihispania la kundi la Boran, ambalo linajumuisha tabaka kubwa la lugha la Witotoan.
Bobana Oromo ambao pia huitwa Boran ni jamii ipatikanayo Kusini mwa Ethiopia, Oromai na Kaskazini mwa Kenya[1] ambao wanajulikana kuwa wafugaji. Wao ni Kundi dogo la Oromo[2]. Wanawakilisha nusu ya makundi mawili ya Waoromo wa Kiasili, nusu nyingine ikiwa Barentu.
Yaliyomo |
Wasifu [hariri]
Waoromo wa Kaskazini mwa Kenya waliingia eneo hilo mara ya Kwanza kutoka Kusini mwa Ethiopia wakati wa uhamizi mkubwa wa Karne ya Kumi. Walitawanyika kuwa Waborana wafuga Ng'ombe na wafuga Ngamia, Wagabra na Wasakuye[3].
Lugha [hariri]
Waborana huzungumza Kiborana (au afaani Boraana), ambayo ni mojawapo ya sehemu ya Kushaiti (Cushite) ambayo pia ni mojawapo ya kundi kubwa la Afro-Asiatic. Takribani watu milioni 7 wanajitambulisha na jamii ya Borana.
.
Kalenda ya Kiborana [hariri]
Inaaminika kuwa Waborana wana Kalenda yao waliyoitunga karibu miaka ya 300 BC. Kalenda yao ni mfumo wa lunar-stellar, ambayo hutegemea matukio ya anga ya mwezi pamoja na Nyota Saba. Miezi ya Kiborana (Mizunguko ya miezi na nyota) ni: Bittottessa (iangulum), Camsa (Pleiades), Bufa (Aldebarran), Waxabajjii (Belletrix), Obora Gudda (Orion-Saiph ikiwa kati), Obora Dikka (Sirius), Birra (Mwezi mzima), Cikawa (gibbous moon), Sadasaa (Nusu-mwezi), Abrasa (Kipande kikubwa cha mwezi), Ammaji (Kipande cha wastani), na Gurrandala (Kipande kidogo)[4].
Matabaka madogo [hariri]
Waoromo wanjumuisha makundi mawili muhimu, ambayo hugawanyika katika koo nyingi za kifamilia. Kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na Kaskazini kuelekea Kusini, matabaka hayo ni:
- Macha Oromo waishio katikati ya mito ya Didessa na Omo, na kusini kuelekea Gibe;
- Tulama Oromo, waishio Oromia, karibu na Addis Ababa;
- Guji Oromo, kundi la Kusini la Oromo, wanaoishi karibu na Garri na Borana Oromo
- Borana Oromo, waishio katika eneo la Borena Zone, ambayo inajumuisha Moyale. Wanaishi pia nchini Kenya na sehemu za somalia.
- Gabra Oromo ambao wanaishi Kaskazini mwa Kenya katika Mpaka wa Moyale eneo la Garri, (Gharri)[clarification needed], ambao wanaishi Kaskazini Mashariki mwa Kenya na sehemu za Somalia
...Na vijikundi vingi vingine
Tazama Pia [hariri]
Vidokezo [hariri]
- ↑ Ethnologue;Ethnologue
- ↑ Aguilar, Mario. The Eagle as Messenger, Pilgrim and Voice: Divinatory Processes among the Waso Boorana of Kenya. Journal of Religion in Africa, Vol. 26, Fasc. 1 (Feb., 1996), pp. 56-72. Rudishwa juu ya 2007-10-27.
- ↑ Elliot M. Fratkin, Eric Abella Roth, As Pastoralists Settle, (Springer: 2005), p.39
- ↑ Lawrence R. Doyle, The Borana Calendar REINTERPRETED
Viungo vya nje [hariri]
Virejeleo [hariri]
| Wikinews has related news: Children massacred in Kenyan school |
- Appiah, Kwame Anthony; Gates, Henry Louis, Jr., eds. (1999), Africana: The Encyclopedia of the African and African American Experience, New York: Basic Books, ISBN 0-465-00071-1, OCLC 41649745.
Kusoma zaidi [hariri]
- Asmerom Legesse, Gada
- Beckingham and G.W.B. Huntingford, Some records of Ethiopia Hakluyt Society, 1954
- Bassi Marco, Decisions in the Shade. Political and juridical processes among the Oromo-Borana Red Sea Press, 2005
- Clifford H F Plowman CMG OBE, Notes On The Gedamoch Ceremonies Among The Boran, (Journal of the Royal African Society, Vol. 18, No. 70 (Jan., 1919), pp. 114–121 )