Marsabit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Marsabit
Marsabit is located in Kenya
Marsabit
Marsabit

Mahali pa mji wa Marsabit katika Kenya

Majiranukta: 2°19′0″N 37°58′0″E / 2.31667°N 37.96667°E / 2.31667; 37.96667
Nchi Kenya
Kaunti Marsabit

Marsabit ni mji wa kaskazini mwa Kenya, kilomita katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ifikapo 37 ° 58 'E, 2 ° 19' N (37,97 ° E, 2.32 N). Karibu pande zote umezungukwa na Mbuga ya Kitaifa ya Marsabit na Hifadhi. Ndio mji mkuu wa Kaunti ya Marsabit, na uko kusini mwa Jangwa la Chalbi katika eneo la misitu inayojulikana kwa milima yake ya volikano na Maziwa yanayopatikana kwenye kilele cha milima.

Mji wa Marsabit[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Marsabit ndio wa ustaarabu katika eneo kubwa ya ukame ya kaskazini mwa Kenya. Mji huu uko juu ya volkano ya kipekee isiyo lipuka, Mlima Marsabit, ambayo ina urefu wa karibu kilomita moja juu ya bahari ya mchanga wa jangwa. Milima iliyo hapa iko na wingi wa misitu, kinyume na jangwa iliyo karibu, pamoja na "Visiwa" vyao vya mfumo wa uhusiano baina ya viumbe.

Mji huu unakaliwa na wakaazi wenye asili ya Nilotic ambao ni Samburu na Turkana, pamoja na wakaazi wenye asilia ya Cushitic kama vile Gabbra, Burji,Borana na Rendille. Pia ni nyumbani kwa baadhi ya wafanyibiashara na wahamiaji wa Kisomali.

Aidha, Marsabit ina kiwanja kidogo cha ndege na kilele mlima (Mlima Marsabit), na visima vya "kuimba" nje ya mji. Ndovu pia wanaweza mara nyingi kuonekana katika hifadhi ya wanyamapori inayozunguka mji huu, mara kwa mara zikivunja ua na kusababisha uharibifu wa mazao ya wakulima wenyeji.

Jina la mji linatokana na neno la Kiamhariki 'Marsa bet' (Maana yake nyumba ya au nyumbani kwa Marsa) inaaminika kuwa uliitwa baadaa ya mkulima aitwaye 'Marsa' (wa kabila la Burji) aliyeletwa Marsabit kutoka Mega (nchini Ethiopia) na Consul kusaidia katika kuimarisha kilimo na makaazi ya kudumu kwenye mteremko wa Mlima Marsabit.

Utamaduni na dini[hariri | hariri chanzo]

Ngamia zikikunywa maji katika Marsabit mwaka wa 2005

Kando na makabila yaliyo tajwa hapo mbeleni, kuna watu wengine kutoka maeneo mengine ya Kenya wanaofanya kazi sana sana za serikali na biashara. Karibu 40% ya watu wanaoishi mjini Marsabit ni Wakristo, 32% Waislamu na wengine 28% huamini katika dini ya jadi na zinginezo. Kwa muda mwingi, makundi haya yameishi kwa amani, lakini tangia mwaka wa 1994 na kudumu kwa karibu mwaka, kulikuwa na mauaji ya kikabila dhidi ya Gabra na Borana, kufuatia mgogoro juu ya umiliki wa mifugo na kila kabila - ambayo ni chanzo cha mapato kwa makundi yote mawili, kando na biashara ya bidhaa na vyakula.

Marsabit ndio eneo lililotangazwa la mkutano kati ya wazee wa Gabra na Borana uliopangwa kufanyika tarehe 2-6 Juni 2009. Mijadala ya kutatua migogoro iliyopo kati ya makundi mawili imekuwa ikiendelea kwa miaka kadhaa sasa, na mikataba inatarajiwa kukubaliwa kwenye tukio hili la mkutano huu mbele ya viongozi wa jadi.[1]

Uchukuzi[hariri | hariri chanzo]

Marsabit ipo takriban kilomita 550 au siku mbili kwa gari kutoka Nairobi kupitia miji ya Isiolo na Archer's Post, kwa kutumia aidha matatu au usafiri wa binafsi. Kuna uwanja mdogo wa ndege unaoshughulikia ndege za kukomboa.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Marsabit ni kituo cha biashara ,kukiweko pamoja na vituo vitatu vya petroli , benki, posta, maduka, mikahawa, majumba ya kulala na hata dobi. Mji huu unawezesha ubadilishanaji na uchukuzi wa bidhaa na huduma kati ya Moyale (bidhaa kutoka Ethiopia) na Isiolo (bidhaa kutoka Nairobi). Kilimo pia kina jukumu, kwani wakaazi wengi hupanda mtama na mahindi kwa kuliwa na wenyeji na wafugaji wa kuhamahama huleta nyama kwa kuuza ng'ombe wao.

Ziwa Paradiso (linalovutia wanyamapori kama ndovu na nyati), na Bongole Crater yaliyoko katikakati mwa msitu , yote ni vivutio kwa watalii wa ndani. Mji huu na maeneo yanayozunguka yana utajiri mkubwa wa utamaduni kwa waanthropolojia na watafiti wengine.

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Borana and Gabra peace meeting in Dukana", Archived 30 Machi 2009 at the Wayback Machine. Pastoralists Communication Initiative website (accessed 5 Mei 2009)

Coordinates: 2°20′N 37°59′E / 2.333°N 37.983°E / 2.333; 37.983