Samos
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samos ni kisiwa cha Ugiriki kilichopo kilomita 1.3 mbele ya pwani la Uturuki. Ni pia moja ya wilaya 51 za Ugiriki.
Samos ina urefu wa 44 km na upana wa 19 km, eneo lake ni 477 km². Sehemu kubwa ni milima inayofikia kimo cha 1,153 m.
Kuna wakazi 33,800 na mji mkubwa unaitwa Samos vilevile ina watu 6,000. Uchumi unategemea utalii pamoja na kilimo. Divai ya Samos ni maarufu.
Katika historia ya Ugiriki ya Kale Samos ilikuwa nyumbani kwa wataalamu mashuhuri kama Pythagoras, Epikuri na Herodoti.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Samos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikimedia Commons ina media kuhusu: