Prince Kagwema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Prince Kagwema (alizaliwa katika kijiji kilichopo mashariki mwa wilaya ya Rungwe, mwaka 1931) ni mwandishi wa Tanzania.

Alijifunza masomo ya lugha ya Kiingereza na Historia katika Chuo Kikuu cha Makerere na kupata shahada, pia aliwahi kufanya mtihani wa Chuo Kikuu cha Cambridge, kati ya miaka 1958 na 1976; alifanya kazi katika shirika la reli East African Railway Corporation katika jiji la Nairobi; baada ya hapo alikwenda kuishi katika jiji la Dar es Salaam.

Prince Kagwema alichapisha kitabu cha riwaya kilichoitwa Veneer of Love kilichotoka mwaka 1975, na riwaya nyingine iliyoitwa Married Love is a Plant kilichotoka mwaka 1983. Mwaka 1983 alitoa riwaya nyingine iliyoitwa Chausiku's Dozen, na Society in the Dock kilichotolewa mwaka 1984, tena mwaka 1985 alichapisha kitabu kilichoitwa Fear of the Unknown - Quo vadis Tanzania?.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Prince Kagwema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.