Ndimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ndimu

Ndimu, mbichi (sehemu zinazoliwa) Virutubisho kwa gramu 100 (3.5 oz) Nishati 126 kJ (30 kcal) Kabohaidreti 11 g Sukari 1.7 g Makapi 3 g Fati 0.2 g Protini 0.7 g Maji 88 g Vitamini C 29 mg (48%)


Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Ndimu ni neno ambalo linatumika kuelezea matunda ya aina mbalimbali, spishi na uzao mbalimbali; mimea ya jamii ya michungwa ambayo yote asili yake ni maeneo ya Himalaya huko India. Umbo lake ni mduara rangi yake ni kijani mpaka manjano, na kipenyo cha sm 3 mpaka 6 lenye ladha ya uchachuna aside ndani yake. Ndimu mara nyingi hutumika kuongeza ladha kwenye chakula na vinywaji. Kwa kawaida ni ndogo kuiko limao, na chanzo kizuri pia cha vitamin C. Ndimu hulimwa mwaka wote na huwa tamu kuliko limao. Ndimu ni matunda madogo, ambayo ngozi na nyama yake ni kati ya inchi moja au mbili hivi. Ndimu huweza kuwa chungu au tamu. Ndimu chungu huwa kiasi kikubwa cha sukari na asili ya asidi citric kuliko malimao na kuwa na ladha ya asili huku ndimu tamu hukosa asidi ndani yake hivyo kuwa na ladha tamu kweli kweli.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kupikia[hariri | hariri chanzo]

CDC.jpg Katika mapishi ndimu huthaminiwa kwa yote , ladha yake ya aside na harufu yake ya kukoza ni viungo maalumu sana kwa vyakula vya Meksiko, Vietnamu, Thailandi na kusini mashariki mwa Marekani. Zaidi hata majani ya mmea wa ndimu hutumika kwenye mapishi hasa katika nchi za Asia. Majani ya mmea huu hutumika kama dawa pia katika maeneo mengi hasa kusini na mashariki mwa Asia .

Matumizi mengine[hariri | hariri chanzo]

Katika kutibu ugonjwa wa ngozi, kiseyeye mnamo karne ya 19, serikali ya Uingereza ilihimiza watu wale sana ndimu, hii ni kutokana na kuwa chanzo kizuri cha vitamini C. Pamoja na mafuta maalumu, maji ya limao pia hutoa mchanganyiko unaotumika katika matengenezo ya marashi. Baadhi ya watu hunyunyiza maji ya ndimu kwenye macho yao, kupata uoni mzuri. Huko India hutumika kuwekwa kwenye imani yao kufukuza roho wabaya.

Uzalishaji[hariri | hariri chanzo]

India inaongoza kwa kuzalisha kwa wingi malimao na ndimu kwa wingi zaidi kwa asilimia 16, ikifuatwa na Meksiko (14. 55%), Ajentina (10%), Brazili (85%) na Hispania (7%)