Limau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Limau nzima na limau nusu
Limau bivu na ua lake

Limau (pia: limao; kutoka Kar. ليمون limun) ni tunda la mlimau. Pamoja na chungwa, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa.

Rangi ya tunda lililoiva ni njano hadi njano-kijani. Maji yake ina asidi nyingi na ladha yake ni chungu. Matumizi yake ni katika upishi hasa na tunda haliliwi moja kwa moja kutokana na uchungu mkali. Maji yake hutumiwa kwa ajili ya vinywaji ama kama kiungo pamoja na majiy a matunda mengine au mara nyingi kwa kuongeza sukari na maji.

Limau ina vitamini C nyingi ndani yake na kiasi kidogo kinatosheleza mahitaji ya kibinadamu. Sifa hii ilitambuliwa wakati mabaharia kwenye jahazi walipata ugonjwa wa kiseyeseye uliokuwa balaa kwa safari za kwanza zilizovuka bahari za Atlantiki na Pasifiki wakati wa upanuzi wa Wareno, Wahispania na Waingereza kuanzia karne ya 16. Hapa limau zilitambuliwa kuwa dawa lililozuia ugonjwa huu kutokana kiasi chacke cha vitamini C.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Greentree.jpg Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Limau kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.