Chungwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Machungwa na maua yake
Chungwa bivu

Chungwa ni tunda la mchungwa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck.

Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. Siku hizi ni tunda linalovunwa zaidi kati ya matunda chungwa.

Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima. Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu.

Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina tamu.

Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15.

[hariri] Nchi za mavuno

Nchi za mavuno — 2005
(tani milioni)
Brazil 17.8
Marekani 8.4
Mexiko 4.1
Uhindi 3.1
China 2.4
Hispania 2.3
Italia 2.2
Uajemi 1.9
Misri 1.8
Pakistan 1.6
Dunia yote 61.7
Chanzo:
FAO
[1]



[hariri] Viungo vya Nje


Cite error: <ref> tags exist, but no <references/> tag was found