Kikoongo
Kikoongo (pia: Kikongo) ni lugha ya Kibantu hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako inahesabiwa kati ya lugha 4 za kitaifa. Kinazungumzwa na Wakoongo. Idadi ya wasemaji wa Kikoongo kama lugha ya kwanza katika Jamhuri imehesabiwa kuwa watu milioni tatu; pamoja na hayo kuna watu milioni tano ambao huongea Kikoongo kama lugha ya pili. Tena kuna wasemaji wa Kikoongo milioni moja nchini Angola na milioni moja nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikoongo kiko katika kundi la H10.
Viungo vya nje [hariri]
- lugha ya Kikoongo kwenye Multitree
- ramani ya Kikoongo
- http://www.ethnologue.org/show_language.asp?code=kng
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.