Jumapili ya matawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jumapili ya matawi ikiadhimishwa na Waorthodoksi wa Biškek huko Kirghizistan.

Katika mwaka wa Kanisa wa madhehebu mbalimbali ya Ukristo, Jumapili ya matawi inaadhimishwa jinsi Yesu Kristo alivyoingia Yerusalemu ili kufa na kufufuka kwa wokovu wa binadamu wote. Siku hiyo alishangiliwa na umati kwa kutumia matawi, ndiyo asili ya jina.

Ndiyo mwanzo wa Juma kuu linaloadhimisha matukio makuu ya historia ya wokovu kadiri ya imani ya Wakristo.

Tangu mwaka 1985 siku hiyo Kanisa Katoliki linaadhimisha pia "Siku ya kimataifa ya vijana".