Nenda kwa yaliyomo

Gabriel Zubeir Wako

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kardinali Wako.

Gabriel Zubeir Wako (kwa Kiarabu: غبرايل زوبير واكو; alizaliwa Mboro, Sudan, tarehe 27 Februari 1941) ni askofu mkuu wa Kanisa Katoliki aliyechunga jimbo kuu la Khartoum, Sudan.[1]

Alipata upadirisho tarehe 21 Julai 1963, akawa askofu wa jimbo la Wau mwaka 1974, halafu askofu mkuu wa Khartoum mwaka 1981.

Gabriel Zubeir Wako aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa kardinali-padri wa parokia ya Sant'Atanasio a Via Tiburtina' tarehe 21 Oktoba 2003.

Ni kati ya makardinali walioshiriki uchaguzi wa Papa Benedikto XVI mwaka 2005 na wa Papa Fransisko mwaka 2013.

Kardinali Zubeir Wako alinusurika kuuawa wakati wa kuadhimisha Misa ya Jumapili tarehe 10 Oktoba 2010.[2] [3]

Tarehe 10 Desemba 2016 aling'atuka na kurithiwa na Askofu Mwandamizi Michael Didi Adgum Mangoria.[4]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • "Zubeir Wako Card. Gabriel". Holy See Press Office. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)


  1. "Gabriel Cardinal Zubeir Wako". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-23. Iliwekwa mnamo 2011-06-29.
  2. https://www.indcatholicnews.com/news/16900
  3. "Christian leader narrowly escapes Muslim assassination attempt". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-14. Iliwekwa mnamo 2011-06-29.
  4. "Other Pontifical Acts". Iliwekwa mnamo 2016-12-10.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.