Fransisko Solano
Fransisko Solano, O.F.M. (Montilla, Córdoba, 10 Machi 1549 - Lima, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Hispania alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini na hatimaye kufariki katika mji mkuu wa Peru ya leo.
Jina lake kwa kirefu lilikuwa (Kihispania: Francisco Sánchez-Solano Jiménez).
Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai.
Yaliyomo |
Heshima baada ya kifo [hariri]
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.
Sala yake [hariri]
Yesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!
Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?
Nina thamani gani usipokuwa nami?...
Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.
Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...
Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?
Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?
Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...
Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!
Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!
Marejeo [hariri]
This article incorporates text from a publication now in the public domain: Herbermann, Charles, ed (1913). "St. Francis Solanus". Catholic Encyclopedia. Robert Appleton Company.
Viungo vya nje [hariri]
- Francis Solano at Patron saints Index
- St. Francis Solano at "Saints Alive"
- (Kihispania) San Francisco Solano
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fransisko Solano kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |