Bahari ya pembeni
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya pembeni ni sehemu ya bahari kubwa fulani inayotengwa nayo kwa kisi fulani kwa nchi kavu kama rasi, visiwa au funguvisiwa pamoja na miinuko iliyopo chini ya maji.
Mifano michache ni:
Bahari za pembeni za Atlantiki
- Mfereji wa Kiingereza
- Bahari ya Eire (imetengwa na Eire na Britania)
- Bahari ya Kaskazini (imetengwa na Britania)
- Bahari ya Mediteranea (imeunganishwa na Atlantiki kwa mlango wa Gibraltar pekee)
Bahari za pembeni za Mediteranea
- Bahari Nyeusi (imetengwa na Uturuki)
- Bahari ya Marmara
Bahari za pembeni za Bahari Hindi:
- Ghuba ya Uajemi (imetengwa na Uarabuni)
- Bahari ya Shamu (imetengwa na Uarabuni)
Bahari za pembeni za Pasifiki:
- Bahari ya Kusini ya China (imetengwa na Indonesia na Ufilipino)
- Bahari ya Japani (imetengwa na visiwa ya Japani)