Mlango wa Gibraltar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya chombo cha angani
Sehemu nyembamba ya mlango karibu na rasi ya Gibraltar
Moroko inavyoonekana ng'ambo ya mlango wa Gibraltar

Mlango wa Gibraltar ni mlango wa bahari kati ya Moroko na Hispania. Unaunganisha bahari za Atlantiki na Mediteranea. Ni mahali ambako bara za Afrika na Ulaya ziko karibu.

Mlango wa Gibraltar una upana kati ya 44 km hadi 14 km. Urefu wa sehemu nyembamba ni takriban 60 km. Kina cha maji hufikia 286 m.

Pwani la kaskazini ni eneo la Hispania isipokuwa rasi ya Gibraltar ambayo ni eneo la ng'ambo la Uingereza. Pwani la kusini ni Moroko isipokuwa eneo dogo la mji wa Kihispania wa Ceuta.

Jina la Gibraltar[hariri | hariri chanzo]

Jina la Gibraltar limetokana na uvamizi wa Waarabu wakati wa upanuzi wa Uislamu. Mwaka 711 jemadari Tariq ibn-Ziyad aliongoza jeshi lake kushambulia Hispania. Rasi inayoitwa leo "Gibraltar" ilipewa jina la "jabal at-Tariq" (mlima wa Tariq) lililokuwa baadaye "Gibraltar". Kabla ya kuja kwa Waarabu mataifa ya kale yaliita mlango huu "Nguzo za Herakles" wakitaja milima midogo ya Gibraltar na Ceuta kwa jina hili.

Mikondo ya juu na chini[hariri | hariri chanzo]

Zamani za jahazi mlango ulikuwa njia ngumu sana. Kuna mkondo mkali kutoka Atlantiki ambamo maji mwepesi ya Atlantiki huingia katika Mediteranea. Wataalamu waligundua baadaye ya kwamba kuna mkondo mwingine kinyume chake wa kutoka katika Mediteranea. Maji yenye chumvi na hivyo uzito zaidi hutoka kwenye kina cha takriban 100 m chini ya UB. Wataalamu kati ya nahodha wa kale walitumia nanga ya kuelea chini ya maji iliyofikia kina hii kama aina ya injini ya kuvuta jahazi dhidi ya mkondo wa juu.

Mlango wa Gibraltar ni kati ya njia za bahari zinazotumiwa sana na meli. Kwa wastani kuna meli 300 zinazopita humoi kila siku.

Mipango ya daraja[hariri | hariri chanzo]

Kuna mipango ya kuunganisha Afrika na Ulaya kwa reli au barabara. Hadi sasa hakuna uamuzi bado.