Visiwa vya Falkland
|
|||||
| Wito la taifa: "Desire the right" | |||||
| Wimbo wa taifa: "God Save the Queen" | |||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Stanley |
||||
| Mji mkubwa nchini | Stanley | ||||
| Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
| Serikali | Eneo la ng'ambo la Uingereza Queen Elizabeth II |
||||
| Eneo la ng'ambo la Uingereza Siku ya uhuru (Ushindi juu ya Argentina) |
14 Juni 1982 | ||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
12,173 km² (162) 0 |
||||
| Idadi ya watu - Julai 2008 kadirio - Msongamano wa watu |
3,140 [1] (217) 0.26/km² (240) |
||||
| Fedha | Falkland Islands pound (FKP) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC-3) |
||||
| Intaneti TLD | .fk | ||||
| Kodi ya simu | +500
|
||||
Visiwa vya Falkland (Kiingereza: Falkland Islands au Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban 450 km mbele ya pwani la Argentina.
Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake.
Funguvisiwa ina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban 6,000 km². Mwinuko mkubwa ni mlima wa Mount Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) mwenye 708 mita juu ya uwiano wa bahari.
Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hii mimea ni hasa manyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.
Idadi ya wakazi haizidi 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki yao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo. Mji wa pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki mwenye wakazi 2100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500. Barabara ya lami ya pekee kisiwani inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.
Argentina inadai ya kwamba visiwa ni eneo lake na 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita fupi ya wiki 6 Argentia ilishindwa; takriban wanajeshi 1000 waliuawa.
Viungo vya Nje [hariri]
- ↑ Falkland Islands (Islas Malvinas). CIA. Rudishwa juu ya 2010-03-05.
- L.L. Ivanov et al.. The Future of the Falkland Islands and Its People. Sofia: Manfred Wörner Foundation, 2003. 96 pp. ISBN 954-91503-1-3 (Capítulo principal en español)
- Carlos Escudé y Andrés Cisneros, dir. Historia general de las relaciones exteriores de la República Argentina. Obra desarrollada y publicada bajo los auspicios del Consejo Argentino para las Relaciones Internacionales (CARI). Buenos Aires: GEL/Nuevohacer, 2000. ISBN 950-694-546-2 (en castellano)
- Graham Pascoe and Peter Pepper. Getting it right: The real history of the Falklands/Malvinas. Mei 2008.
- D.W. Greig, Sovereignty and the Falkland Islands Crisis. Austrialian Year Book of International Law. Vol. 8 (1983). pp. 20-70. ISSN: 0084-7658
- http://www.pcgn.org.uk/Falkland%20Islands-July2006.pdf
