Evening Times

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Evening Times
Eveningtimes.jpg
Jina la gazeti Evening Times
Aina ya gazeti * Gazeti la kila siku
* Toleo la Late News Edition
* Toleo la
Late News Extra
Lilianzishwa 1876
Nchi Scotland
Mhariri Donald Windsor Martin
Mmiliki Newsquest
Makao Makuu ya kampuni 200 Renfield Street
Glasgow
Nakala zinazosambazwa 68,422
Machapisho husika * The Herald
Tovuti http://www.eveningtimes.co.uk

/pre>

Historia[hariri | hariri chanzo]

The Evening Times ni gazeti linalochapishwa kutoka Jumatatu hadi Jumamosi jijini Glasgow, Scotland.

Jarida hili, gazeti dada la The Herald, lilianza kuchapishwa katika mwaka wa 1876. Kaulimbiu yake ni "Nobody knows Glasgow better" ("Hakuna mtu anayejua Glasgow zaidi").

Uchapishaji wa Evening Times(na gazeti dada lake) ulihamia jengo la Charles Rennie Mackintosh katika barabara ya Mitchell Street katika mwaka wa 1868. Jengo hili ,hivi sasa, linaitwa The Lighthouse na ni Kituo cha Scotland cha Uchoraji wa Majengo na Ubunifu wa mitindo ya kujenga majumba ya jiji.

Katika mwaka wa 1964, kampuni ya uchapishaji ya George Outram ilinunuliwa na Sir Hugh Fraser. Ulipofika mwaka wa 1979, umiliki ulichukuliwa na kampuni ya Lonrho ya Tiny Rowland.

Tarehe 19 Julai 1980, jarida hili lilihamia ofisi katika barabara ya 195 Albion Street, jumba lenyewe lilikuwa na pande ya mbele iliyokuwa rangi nyeusi hasa likifuata mtindo wa jengo la Black Lubyanka la gazeti la Daily Express lililokuwa katika barabara ya London ya Fleet Street. Jengo hilo la Albion Street lilikuwa limetumika kama jumba la shirika la wafanyikazi wa gazeti la Scotland la Daily News tangu Mei hadi Novemba 1975.

Usimamizi ulinunuliwa mnamo Mei 1992 na Caledonian Newspapers ikaundwa, kampuni hii ilinunuliwa baadaye na stesheni ya televisheni ya Scotland Television katika mwaka wa 1996. Baada ya ununuzi huu, kundi hilo la televisheni lilijiita Kundi la "Scottish Media Group", jina hili lilifupishwa kuwa SMG na na hapo mwaka wa 2008 likaitwa STV Group plc.

Magazeti ya The Evening Times na The Herald yanamilikiwa na Newsquest (sehemu ya kampuni ya Gannett),iliyonunua sekta ya uchapishaji ya SMG katika mwaka wa 2003 kwa bei ya £ milioni 216. Bei hiyo iliyoleta uzushi sana.

Gazeti hili huuzwa katika maduka yake maalum karibu na Glasgow City Centre, wauzaji wakinena kaulimbiu inayojulikana ya Times!'Evening Times!' kila dakika chache. Aidha, husambazwa hadi kwa milango ya nyumba za watu na wavulana na wasichana wanaofanya kazi hiyo na ,pia, huuzwa katika maduka mengi ya Glasgow.

The Evening Times linapatia jina lake chapisho dogo la kila mwaka la kandanda ya Scotland linaloitwa Wee Red Book. Chapisho hili huorodhesha michuano ya timu inayofanyika mwaka huo katika ligi zote za Scotland na huorodhesha washindi wa hapo awali katika ligi na mashindano ya kombe nchini Scotland,Uingereza na Uropa.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]