Lincolnshire Echo
Lincolnshire Echo | |
---|---|
Jina la gazeti | Lincolnshire Echo |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la kila siku *. Gazeti la asubuhi *. Gazeti la Jumatatu mpaka Jumamosi |
Lilianzishwa | 1894 |
Eneo la kuchapishwa | Katika au karibu na Lincoln |
Nchi | Uingereza |
Mhariri | Jon Grubb |
Mmiliki | Northcliffe Newspapers |
Mchapishaji | Kampuni ya Northcliffe Newspapers |
Makao Makuu ya kampuni | Sheffield |
Nakala zinazosambazwa | Takriban magazeti 20,181 |
Machapisho husika | Magazeti ya Target |
Tovuti | http://www.thisislincolnshire.co.uk/ |
Lincolnshire Echo ni gazeti la asubuhi la kila siku la Uingereza la eneo la Lincolnshire. Lilianzishwa katika mwaka wa 1894 na huchapishwa tangu Jumatatu mpaka Jumamosi. Linamilikiwa na kampuni ya Northcliffe Newspapers. Maeneo makuu ya usambazaji wa jarida hili ni katika au karibu na Lincoln.
Katika mwaka wa 2005, kiwanda cha uchapishaji cha Lincoln kilifungwa na uchapishaji kuhamishwa kutoka Grimsby na kisha kuhamishwa Derby. Huchapishwa mara kwa mara huko Stoke. Kutokana na hayo, gazeti hili huchapishwa mapema sana asubuhi na huwa tayari kuuzwa tangu saa 7 asubuhi. Hakuna uchapishaji wa toleo la pili na gazeti hili hutumia tovuti kutangaza habari mpya zilizotokea katika siku kucha. Jumba la Lincolnshire Echo liliuzwa Aprili 2009 kwa Chuo Kikuu cha Lincoln. Lincolnshire Echo lilihamisha ofisi zake hadi Witham Wharf, bado katikati mwa jiji.
Kampuni ya Lincolnshire Media Ltd huchapisha mfululizo wa magazeti mbalimbali ya Target - ambayo ni magazeti ya bure ya kila wiki yaliyo na makala yaliyokuwa katika Echo yaliyopita. Huwa ya maeneo maalum kama yale ya Boston, Gainsborough, Grantham, Lincoln, Louth na Skegness. Retford Times ni gazeti la kila wiki la kulipiwa la mji wa Retford, huchpishwa pia na kampuni ya Lincolnshire Media. Kampuni hii huwa na tovuti: thisislincolnshire.co.uk na sportsecho.co.uk - tovuti ya michezo iliyochukua nafasi ya jarida la michezo la Jumamosi lililofungwa katika mwaka wa 2006.
Gazeti la Echo lina usambazaji wa takriban magazeti 20,181 ingawa magazeti ya Target yana usambazaji wa magazeti mengi zaidi.
Gazeti hili lilivishwa taji la "Gazeti la Maeneo la Mwaka" na muungano wa Newspaper Society katika mwezi wa Aprili 2005. Mhariri wa sasa ni Jon Grubb.
Shida za kiuchumi na mabadiliko ya kitabia yalisababisha faida za kampuni mzazi ya Lincolnshire Echo kushuka kwa asili mia 91.
Katika kipindi cha miaka ya 2002 na 2005 , jarida hili lilikuwa na jukumu kubwa katika kufichua kashfa ya kisiasa katika eneo lake. Lilimfichua Jim Speechley, aliyekuwa kiongozi wa Linncoln County Council, kwa kuonyesha kuhusika kwake katika ufisadi wa fedha na hivyo basi akafungwa jelani kwa miezi 18 katika mwaka wa 2004.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- http://www.nsdatabase.co.uk/newspaperdetail.cfm?paperid=607 Ilihifadhiwa 25 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- http://mediapack.lincolnshireecho.co.uk/awards/?genid=1556&homeid=1495&pageno=1&subcentreid=17 Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- http://www.pressgazette.co.uk/search_results.asp?refresh=0&keyword=Northcliffe&searchtype=kyphase&mags=1&&resorder=0&imageField.x=24&imageField.y=10 Ilihifadhiwa 19 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/campaigns/2002/05may/020509linc.shtml Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/CAMPAIGNS/2004/04apr/040430go.shtml Ilihifadhiwa 26 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/news/2004/04apr/040406ro.shtml Ilihifadhiwa 20 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/news/2004/04apr/040406ech.shtml Ilihifadhiwa 20 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/NEWS/2004/05may/040520or.shtml Ilihifadhiwa 20 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.holdthefrontpage.co.uk/news/2005/03mar/050323lin.shtml Ilihifadhiwa 20 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.