Western Mail (Wales)
Western Mail | |
---|---|
Jina la gazeti | Western Mail |
Aina ya gazeti | Gazeti la kila siku |
Lilianzishwa | 1869 |
Eneo la kuchapishwa | Wales |
Nchi | Wales |
Mmiliki | Trinity Mirror |
Makao Makuu ya kampuni | *. Six Park Street *. Cardiff |
Nakala zinazosambazwa | 32,926 (Agosti 2009) |
Tovuti | http://www.walesonline.co.uk/ |
Western Mail (Swahili: Barua ya Magharibi) ni gazeti la kuchapishwa kila siku na kampuni ya Media Wales katika mji wa Cardiff, Wales. Kampuni hii inamilikiwa na kampuni kubwa kabisa ya magazeti ya Uingereza, kampuni ya Trinity Mirror.
Ingawa gazeti hili hujitambulisha kama "gazeti la taifa la Wales" ( hapo awali lilitangaza "gazeti la taifa la Wales na Monmouthshire") , gazeti hilo lina usambazaji mdogo sana katika eneo la Wales Kusini. Jarida hili lilichapishwa katika mtindo mpana hadi mwaka wa 2004 lilipoanza kuchapishwa kwa mtindo mdogo.
Western Mail lilianzishwa katika eneo la Cardiff katika mwaka wa 1869 na John Crichton-Stuart kama gazeti (bei la peni moja) la kuchapishwa kila siku. Lascelles Carr (1841-1902), mhariri tangu mwaka wa 1869, alinunua gazeti hilo na Daniel Owen katika mwaka wa 1877. Katika historia ya Wales Kusini, Western Mail limehusishwa na wamiliki wa awali, waundaji viwanda vya makaa ya mawe na viwanda vya chuma. Mara nyingi, hii imesababisha jarida hili kusemekana na wengi kuwa ni la kiadui, hasa wakati wa migomo katika viwanda vya makaa ya mawe katika karne ya ishirini. Uhusiano wa zamani wa jarida hilo na wamiliki wa zamani ulikuwa wenye nguvu sana mpaka hivi sasa bado kuna watu katika eneo la Wales Kusini wanaolishuku bado.
Kwa upande mwingine, gazeti hilo limejaribu kuchukua misimamo ya kutetea mitaa, ya watu wengi na ya kutetea Wales huku wakijaribu kuripoti habari zinazohusisha Wales. Gazeti hili husisitiza misimamo yao katika masuala ya kijamii kama kufungwa kwa shule za Wales. Pia, huwasilisha habari nyingi kuhusu timu za Wles za mchezo wa raga.
Jarida hili lina nafasi gazetini inayopewa makala ya lugha ya Kiwales katika toleo lolote la gazeti hili. Habari katika lugha ya Kiwales hupewa kurasa mbili katika toleo la Jumamosi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Audit Bureau of Circulation: Summary Report - The Western MailArchived 15 Aprili 2012 at the Wayback Machine.
- Minutes of the Welsh Local Government Association Co-ordinating Committee, 26 Machi 2004 Archived 17 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- The Welsh Academy Encyclopaedia of Wales. John Davies, Nigel Jenkins, Menna Baines and Peredur Lynch (2008) pg615 ISBN 978-0-7083-1953-6
- Harry Kretchmer (Julai 19, 2002). "Closing doors for the last time". Western Mail: p. 3 (features)