Nenda kwa yaliyomo

Northamptonshire Evening Telegraph

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Northamptonshire Evening Telegraph
Jina la gazeti Northamptonshire Evening Telegraph<vr> *. Jina la utani: ET
Aina ya gazeti *. Gazeti la mtaa
*. Gazeti la Jumatatu hadi Jumamosi
Lilianzishwa 1897
Eneo la kuchapishwa Northamptonshire
Nchi Uingereza
Mmiliki Johnston Press
Northamptonshire Newspapers
Mchapishaji Johnston Press
Nakala zinazosambazwa 22,451 kila siku
Tovuti http://www.northantset.co.uk/

Northamptonshire Evening Telegraph (kwa jina la utani: ET) ni gazeti la mitaa ya upande wa kaskazini wa Northamptonshire likihusisha miji ya Kettering, Corby, Rushden na Wellingborough huko Uingereza. Makao yake yanapatikana katika jumba la Newspaper House katika barabara ya Rothwell Road mjini Kettering ingawa kuna ofisi katika miji yote mitatu.

Gazeti la Evening Telegraph huchapishwa katika rangi zote usiku kucha kutoka Jumatatu hadi Jumamosi. Huchapisha habari za mitaa na michezo haswa kuhusu timu za kandanda za Kettering Town FC (The Poppies ni jina lao la utani), Rushden na Diamonds FC. Gazeti hili limechapishwwa kwa mfululizo tangu 4 Oktoba 1897. Toleo la michezo, Football Telegraph, lilichapishwa hadi mwaka wa 1914 na tena tangu mwaka wa 1921 hadi 1939.

Historia na umiliki

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ya East Midland Allied Press ilianzishwa katika mwaka wa 1947 kutokana na muungano wa kampuni za Northamptonshire Printing and Publishing, Peterborough Advertiser, West Norfolk na King's Lynn Newspaper na sehemu maalum za uchapishaji katika Rushden, King's Lynn na Bury St. Edmunds. Usimamizi ulichukuliwa na Pat Winfrey, mwana wa Bw. Richard Winfrey, aliyekuwa amenunua Spalding Guardian katika mwaka wa 1887. Katika mwaka wa 1996,EMAP, kama kampuni hiyo ilivyojulikana, ilikuwa ikichapisha magazeti 69, gazeti la Northamptonshire Evening Telegraph likiwa miongoni mwao.

Northamptonshire Evening Telegraph na gazeti dada lake, Northampton Chronicle & Echo, hivi sasa yanamilikiwa na kampuni ya Northamptonshire Newspapers Ltd., sehemu ya Johnston Press Plc. Gazeti tofauti la Peterborough Evening Telegraph, linalomilikiwa na kampuni shirika ya Johnston, lilianza kama toleo la mitaa likiwa na kurasa nne za mabadiliko. Kati ya miaka ya 1946 na 1976, matoleo ya maeneo manne tofauti ya kijiografia yalichapishwa yakiwa na kurasa tatu za mabadiliko. Tangu mwaka wa 1988, matoleo ya Kettering, Corby, Wellingborough na East Northants yalianza kuchapishwa tena.

Kampeni na Habari Muhimu

[hariri | hariri chanzo]

Kampeni ya gazeti la Evening Telegraph la mwaka wa 2008 ya kuchanga pesa ilikuwa ikilenga kuchanga £20,000 kwa ajili ya Ambulensi za Warwickshire na Northaptonshire.

Safari ya kikazi ya msichana mwimbaji wa shule, Faryl Smith, ilifuatiliwa na gazeti hili tangu awe umri wa miaka saba. Gazeti hili lilijaribu kumfanyia kampeni ili ashinde mashindano ya Britain's Got Talent(mashindano ya kutafuta talanta mbalimbali) katika mwezi wa Mei 2008. [8]

Tangu 18 Novemba 2008, jarida hili lilichapisha habari kuhusu watu sitini wa Uropa Mashariki ambao walikuwa wameingia nchini humo kwa njia haramu ya kimagendo kisha wakaokolewa na polisi wa Northamptonshire. kufunikwa hadithi ya zaidi ya watu 60 kutoka Ulaya Mashariki aliyekuwa haramu kimagendo ndani ya nchi na amekuwa alituokoa kwa northamptonshire Polisi {0/

Gazeti pia lilichapisha orodha ya heshima ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia - ilihusisha watu wa eneo hilo walioaga dunia katika Vita Kuu.

Lilianzisha kampeni ya Get Active - kampeni ya kufanya watu takriban 20,000 wa eneo la Northamptonshire kuanza kufanya mazoezi ili washinde vifaa vya michezo vya thamani ya paundi milioni moja. [11]

Kampeni nyingine ni ya kuchanga pesa kwa Jenna Mae Tokens, 7, and Chelsea Knighton, 3, ambao walikuwa wakiugua saratani ya watoto.

Kampeni ya Have a Heart - kampeni ya kuchanga £100,000 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya kushughulikia moyo katika hospitali ya Kettering General Hospital.

Kampeni ya Chuo Kikuu ili kupata kampasi katika eneo la kaskazini mwa nchi.

  1. http://www.holdthefrontpage.co.uk/news/080902print.shtml Archived 27 Februari 2009 at the Wayback Machine.
  2. http://www.northantset.co.uk/news/Faryl-chosen-for-Britains-Got.4117717.jp Archived 5 Januari 2009 at the Wayback Machine. - Northants Evening Telegraph
  3. http://www.northantset.co.uk/human/See-inside-the-homes-raided.4704630.jp Archived 14 Novemba 2010 at the Wayback Machine.
  4. http://www.northantset.co.uk/14863/Roll-of-Honour.4799793.jp Archived 13 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
  5. http://www.northantset.co.uk/get/Get-fit-not-fat-in.3618712.jp Archived 17 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
  6. http://www.northantset.co.uk/cherish-chelsea-appeal/Cherish-Chelsea.4635593.jp Archived 2013-04-21 at Archive.today
  7. http://www.northantset.co.uk/news/University-challenge.4020316.jp Archived 26 Aprili 2008 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]