Liverpool Echo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Liverpool Echo
Jina la gazeti Liverpool Echo
Aina ya gazeti *.Gazeti la Jumatatu - Jumamosi
isipokuwa Siku ya Krismasi
*. Gazeti la jioni
Lilianzishwa 1879
Eneo la kuchapishwa Merseyside
Nchi Uingereza
Mhariri Alistair Machray
Mmiliki Trinity Mirror
Makao Makuu ya kampuni Post & Echo Building
Old Hall Street
Liverpool
Nakala zinazosambazwa 110,000 - Jumatatu hadi JumamosiMwaka wa 2007
Machapisho husika *. Gazeti dada:Liverpool Daily Post
Tovuti http://www.liverpoolecho.co.uk/

Liverpool Echo ni gazeti linalochapishwa na kampuni ya Trinity Mirror katika eneo la Merseyside,Uingereza. Linachapishwa katika siku za Jumatatu mpaka Jumamosi, na ni gazeti la jioni la Liverpool na gazeti dada lake , Liverpool Daily Post ni gazeti la asubuhi. Katika nusu ya mwaka wa kwanza wa mwaka wa 2007, Liverpool Echo lilikuwa na usambazaji (wa Jumatatu hadi Jumamosi) wa nakala takriban 110,000.

Hapo awali, gazeti hili lilichapishwa na kampuni ya Liverpool Daily Post & Echo.

Mhariri ni Alistair Machray, aliyekuwa mhariri wa hapo awali wa gazeti la Welsh Daily Post.

Katika mwaka wa 1879, Liverpool Echo lilianza kuchapishwa kama gazeti dada kwa lile la Liverpool Daily Post. Kutoka kuanzishwa kwake hadi mwaka wa 1917, gazeti hilo liliuzwa kwa bei la nusu peni. Hivi sasa bei yake ni 47p.

Kampuni hiyo ilianza kupanuliwa katika mipango ya kuenea kimataifa. Katika mwaka wa 1985, iliendeleza na kuboresha muundo wake na ikaitwa Trinity Holdings Plc. Magazeti haya yalianzishwa tena yakichapishwa katika mitindo ya magazeti ya porojo. Yaliangazia nyakati ngumu za uhaba mkubwa wa ajira na shida za kijamii jijini Liverpool katika mwanzoni wa miaka ya 1980. Katika mwaka wa 1999, kampuni ya Trinity ilijiunga na kundi la Mirror Group Newspapers na kuwa Trinity Mirror. Kampuni hii ikawa kampuni kubwa kabisa ya uchapishaji wa magazeti nchini.

Mnamo Juni 2007, ilitangazwa kuwa gazeti la Liverpool Echo lilikuwa limeshinda haki za kuupa jina uwanja mpya katika eneo la Albert Dock. Hivyo basi, walichagua jina na uwanja huo unajulikana,hivi sasa, kama Liverpool Echo Arena.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]