Herald (Glasgow)
The Herald | |
---|---|
Jina la gazeti | The Herald |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la Jumatatu hadi Jumamosi |
Lilianzishwa | 1783 |
Eneo la kuchapishwa | Nchini Scotland |
Nchi | Scotland |
Mhariri | Charles McGhee |
Mmiliki | Newsquest |
Makao Makuu ya kampuni | *. 200 Renfield Street *. Glasgow |
Nakala zinazosambazwa | *. 55,707 Takwimu za Julai 2009 |
Tovuti | Tovuti Rasmi |
The Herald ni gazeti linalochapishwa Jumatatu hadi Jumamosi jijini Glasgow, na hupatikana kote nchini Scotland. Takwimu za Julai 2009, usambazaji wake ulikuwa nakala 55,707, takwimu hii inaonyesha kuwa gazeti hili linashinda gazeti lile jingine la taifa la The Scotsman katika mauzo.
Muhtasari
[hariri | hariri chanzo]Jarida hili ni mojawapo wa magazeti kongwe ya lugha ya Kiingereza duniani kote. Lilichapishwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1783 kama gazeti la Glasgow Advertiser huko Duncan's Land,Gibson Wynd's, Glasgow. Mhariri wake wa kwanza alikuwa John Mennons.
Katika mwaka wa 1802 likawa gazeti la Herald and Advertiser, likibadilika kuwa Glasgow Herald katika mwaka wa 1805. Lilianza kuchapishwa kila siku katika mwaka wa 1859. Katika mwaka wa 1895, chapisho hilo lilihamia jengo la Charles Rennie Mackintosh katika barabara ya Mitchell Street. Jengo hili sasa ni The Lighthouse, jumba la usanifu na michoro ya majengo.
Katika mwaka wa 1964, kampuni ya uchapishaji ya George Outram ilinunuliwa na Sir Hugh Fraser. Umiliki ,kisha,ulinunuliwa na Lonrho ya Tiny Rowland katika mwaka wa 1979.
Mnamo 19 Julai 1980, jarida hili lihamisha ofisi zake katika barabara ya Albion Street, zilizofanana na jengo la Black Lubyanka ya gazeti la Daily Express lililokuwa katika barabara ya Fleet Street jijini London.
Jarida hili liliitwa jina la The Herald katika tarehe 3 Februari 1992. Usimamizi wake ulinunuliwa katika mwezi wa Mei 1992 na Kampuni ya Magazeti ya Caledonian, kampuni hii ikanunuliwa,hapo baadaye na Scottish Television katika mwaka wa 1996. Baada ya ununuzi huu, kundi hilo la Scottish TV lilijiita jina jipya "Scottish Media Group" (hili lilifupishwa kuwa SMG na katika mwaka wa 2008 likaitwa STV Group plc.).
Kichwa cha gazeti hilo lilichorwa kwa mtindo mpya na gazeti la "New Era" likaanzishwa upya katika mwezi wa 11 Mei 1998. Gazeti shirika la Jumapili , Sunday Herald, lilianzishwa katika mwaka wa 1999.
The Herald inamilikiwa na Newsquest ( kitengo cha kampuni ya Gannett) , iliyonunua kitengo cha uchapishaji cha SMG katika mwaka wa 2006. Ilinunua SMG kwa bei ya £216m katika ununuzi ulioleta migogoro na ubishi.
Waandishi maarufu wa makala ya gazeti hili ni kama: Alison Rowat, Collete Douglas-Hume, Ruth Wishart, Anne Johnstone, Ian Bell, Ron Ferguson, Iain Macwhirter, na Alf Young.
Donald Martin ndiyo mhariri akichukua nafasi ya Charles McGhee katika mwezi wa Desemba 2008. Alianzisha mpango wa kupunguza pesa zilizotumika na kampuni, mpango huo ulipingwa na kuungwa mkono na Bunge la Scotland.
Wahariri
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Phillips, Alastair, (1983). Glasgow's Herald: Two Hundred Years of a Newspaper 1783 - 1983. Glasgow: Richard Drew Publishing. ISBN 0-86267-008-X