Nenda kwa yaliyomo

Ziwa Vostok

Majiranukta: 77°30′S 106°00′E / 77.500°S 106.000°E / -77.500; 106.000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa Vostok
Mahali pa ziwa katika Antaktiki
Mahali pa ziwa katika Antaktiki
Nchi zinazopakana Antaktiki
Eneo la maji km2 12,500
Kina cha chini mita 432
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
,ita -500

77°30′S 106°00′E / 77.500°S 106.000°E / -77.500; 106.000

Ziwa Vostok chini ya barafu ya Antaktiki
Ziwa Vostok jinsi linavyoonekana kutoka satelaiti

Ziwa Vostok ni ziwa lililopo kwenye Bara la Antaktiki chini ya ngao ya barafu. Ni moja kati ya maziwa 400 yaliyotambuliwa chini ya barafu ya Antaktiki; ni ziwa kubwa la bara hilo.

Ni ziwa lenye maji ya kumiminika yaliyo mita 4000 chini ya uso wa barafu ya Antaktiki.

Jina lake limetokana na Kituo cha Vostok cha Urusi kilichopo kwenye uso wa barafu juu yake.

Kuwepo kwa ziwa hilo liligunduliwa na wanasayansi wa Urusi na Uingereza waliotumia mitambo ya rada.

Ziwa lina maji safi. Jotoridi ya maji ni karibu -3 °C lakini hayagandi, hubaki kiowevu kwa sababu ya shinikizo kubwa la barafu juu yake.

Hakuna uthibitisho bado kama huna uhai wowote katika maji ya ziwa hili. Sehemu hii haikuwa na uhusiano na nje kwa miaka milioni kadhaa kwa sababu imefungwa chini ya ngao ya barafu ya Antaktiki. Wanasayansi walitoboa barafu hadi uso wa ziwa mara 3 wakakuta baadaye bakteria katika sampuli za maji lakini imegunduliwa baadaye kwamba bakteria wote ni machafuko yaliyoingizwa na vifaa vya kutobolea barafu. Enzymes ya kinga.

Mazingira katika ziwa yanaaminiwa kufanana na yale ya mwezi Europa wa Mshtarii (Jupiter) au mwezi Enceladus wa Zohali. Kupata uhai katika ziwa hilo kungeongeza uwezekano wa kukuta uhai umekuwepo katika moja ya miezi hiyo. [1]

  1. "Mystery of Antarctica's 15-million year-old lake". The Daily Galaxy. 2007-12-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-16. Iliwekwa mnamo 2009-07-01.

Tovuti za Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.