Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Hamed bin Mohammed el Murjebi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tippu Tip

Hamed bin Mohammed el Murjebi (183714 Juni 1905) amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip. Alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa karne ya 19.

Babake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mamake aliitwa Nyaso. Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo. Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hemed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana.

Hamed akapata jina huko Ulaya kwa sababu alikutana na wasafiri na wapelelezi Wazungu kama David Livingstone, Veney Cameron, Henry Morton Stanley, Eduard Schnitzer (Emin Pascha), Hermann von Wissmann na Wilhelm Junker ambao mara nyingi walipata misaada muhimu kutoka kwake.
►Soma zaidi