Vudee
Vudee ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,114 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,120 [2] walioishi humo.
Kata hii ina vitongoji mbalimbali kama vile Menamo, Ndolwa, Kwanamburi na Kwainga.
Kabla ya uhuru wamisionari kutoka Ujerumani walifika na kueneza dini ya Ukristo, madhehebu ya Kilutheri ambayo hadi leo asilimia zaidi ya tisini na nane ni Walutheri.
Kuna viongozi mbalimbali miaka ya baada ya uhuru tu waliowahi kuchaguliwa kutokea Vudee kama vile aliyewahi kuwa waziri wa elimu, Chediel Mgonja, na aliyewahi kuwa IGP wa pili baada ya uhuru Elangwa Shaidi ambao kwa sasa ni marehemu.
Vudee ilikuwa miongoni mwa vijiji vya Pare Kusini vilivyokuwa na shule ya middle school miaka ya mwisho ya ukoloni; vijana walikuwa wakija kusoma pale wakitokea Chome, Mhezi, Mbaga na sehemu kadha wa kadha za Upare kwa wakati huo.
Wakati huo kulikuwa na watemi Wapare; walikuwa wakiitwa "Vafumwa" kama vile Njaule na wengine wengi.
Enzi hizo kulikuwa na utaratibu maalumu wa kuwaadabisha watu wakorofi kama vile kwa kutohudhuria "Msaragambo" (kazi za kujitolea kwa pamoja) kama vile ujenzi wa shule, kuchimba barabara n.k. Wananchi walikubaliana kuwatoza kuku, mbuzi au kondoo, waliita utaratibu huo "Kupambua" na kazi hii ilikuwa ikifanywa na vijana wenye nguvu. Aliyepambuliwa alitakiwa atimize huo wajibu wake kwa muda maalumu; asipotimiza basi mali yake ilinadiwa na kutunisha mfuko wa kijiji chini ya VDC (Village Development Committee).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta
|