Mshewa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mshewa ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,154 [1] walioishi humo.

Kata ya Mshewa ina vijiji vya Marindi, Mshewa, Manka na Goma.

Mshewa ina ofisi ya kijiji, shule ya msingi, shamba la kilimo na jengo la kahawa linalomilikiwa na Vuaso Cooperative Union.

Pamoja na kanisa la mtaa KKKT usharika wa Marindi, Mshewa kuna Kanisa la Neno na kanisa la EAGT.

Watu maarufu[hariri | hariri chanzo]

Mshewa aliishi Martin Shafuri, mchungaji mwenyeji wa kwanza eneo la Mbaga baada ya wamisionari wa kwanza wa Kilutheri. Mchungaji Shafuri wakati wa kustaafu alipewa kiti kimeandikwa "Ikaa si uheme". Alifariki mwaka 1976.

Karibu na nyumbani kwa Mchungaji Shafuri ametokea mchungaji wa pili hapo Mshewa, Elineema Mwakulala Mndeme ambaye alizaliwa tarehe 24 April 1971. Alibarikiwa kuwa mchungaji tarehe 12 Septemba 1999

Watu maarufu hapo Mshewa ni pamoja na familia ya Simeon Mapande, familia ya Mwang'ombe, familia ya Mchungaji Martin Shafuri, familia ya Lukwaro Wiljohn Mwakulala, familia ya Sheshe, familia ya Timotheo Mnzava, familia ya mzee Fundi, familia ya mzee Kirito, familia ya mzee Hoseni (Kaloko), familia ya Mapande, familia ya Zuberi Mpanga, familia ya Rafaeli Semboja, familia ya mzee Ngwijo, familia ya Solomoni Chazuka na familia ya Enirisha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta|}

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mshewa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.